Katibu Mkuu Chama cha Watu Wenye Ualbino Mkoa wa Dar Es Salaam Gaston Mcheka ametoa shukrani baada ya kupokea vifaa vya kuwasaidia katika shughuli zao za kila siku. Vifaa hivyo ni Mafuta maalum ya kutunza Ngozi, na kofia za kujikinga na mwanga wa jua ambavyo vyote hivyo vimetolewa kama msaada na Meridianbet Tanzania ikiwa ni sehemu ya kuwakumbuka watu mbalimbali wenye mahitaji tofauti kwenye jamii. Akipokea vifaa hivyo Mcheka alibainisha kwamba Meridianbet imesaidia kwa kiasi kikubwa kwani vifaa hivyo vinagharama kubwa sana. “Kiuhalisia haya mafuta yana gharama kubwa sana, ukichukua hii chupa moja ni gharama za chakula kwenye familia kwa milo mitatu, lakini leo hii wenzetu wa Meridianbet wametuletea vingi vya kutosha. Tunawashukuru sana kwa moyo hu una tutakuwa bega kwa began a Meridianbet kwa mambo mengine”- Gaston Mcheka “Lakini mbali na hili nipende kuelezea tena changamoto ya kiyakinishi cha mezani au kiyakinishi mpakato ‘Laptop’ kwa ajili ya kufanyia shughuli zetu za kila ...