Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2020

MADHARA YA VIDONDA VYA TUMBO

  Kama yalivyo magonjwa mengine, vidonda vya tumbo vina madhara endapo havitapatiwa tiba ya uhakika au endapo mhusika atashindwa kufuata maelekezo aliyopewa na daktari kwa ukamilifu wake.  Miongoni mwa madhara yake ni kama yafuatayo: a)        Wakati mwingine husababisha kufanyika kwa upasuaji mkubwa tumboni ili kuondoa eneo lote lililoathirika endapo tatizo halikupatiwa ufumbuzi mapema. b)        Kupungua kwa uwezo wa kufanya tendo la ndoa na hali hii mara nyingi huwakuta wanaume. c)         Uwezo wa kufanya kazi kwa ufasaha hupungua. d)        Kulika kwa utumbo hali inayoweza kupelekea kuvuja damu kwa ndani. e)        Msongo wa mawazo. f)         Kifo  

AMOEBA NI UGONJWA WA TUMBO USIOFAHAMIKA KWA WATU WENGI

W atu wengi wanaugua magonjwa ya tumbo lakini ni wachache wanaofahamu kuhusu ugonjwa wa amoeba unaosababishwa na uchafu wa mazingira, vyombo vya nyumbani ambao huenezwa kupitia bakteria anayejulikana kama Entamoeba histolytica. Vimelea vinavyoenezwa na bakteria huyu humsababishia mtu kuhara haja ambayo huonekana ina kamasi. Ulaji wa matunda bila kuyaosha au kutokunawa mikono baada ya kutoka chooni, kula chakula bila kunawa mikono na kunywa maji yasiyochemshwa zinaelezwa kuwa ni baadhi ya namna zinazosaidia kuwasambaza bakteria hawa hivyo kuenea ugonjwa huu. Mgonjwa hupata maambukizi baada ya kunywa au kula kitu kilichochanganyika na Entamoeba histolytica ambao hukimbilia kwenye utumbo mdogo ambako huzaliana.    Wakiwa wengi, huenda kwenye utumbo mkubwa na kuanza kushambulia mwili. Wakikua, huishi katika kinyesi cha binadamu kisha hutolewa kwa njia ya haja kubwa na kuishi katika ardhi kwa muda wa wiki nne, kipindi ambacho huwa na uwezo wa kusababisha maambuki...