Skip to main content

Sasa ruksa kufanya mikutano ya hadhara- Rais Samia

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Hatimaye kilio cha wanasiasa cha muda mrefu kimepata ufumbuzi baada ya Serikali kuruhusu kuanza kwa mikutano ya hadhara ambayo itazingatia sheria za nchi.

Akizungumza na viongozi wa vyama 19 vya siasa leo Jumanne Januari 3,2023, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa amefurahishwa na kitendo cha mahudhurio ya viongozi wa vyama vya siasa kutoka Tanzania Bara na Visiwani kwani hayo ndiyo aliyokuwa akitaka tangu awali.

Dk. Samia amesema kuwa kuna mambo mengi ambayo awali walizungumza na viongozi wa vyama siasa hivyo bado yanaendelea kufanyiwa kazi na maengine yamefanyiwa kazi.

“Kuna mambo yalizungumzwa na kutakiwa kufanyiwa maamuzi. Busara zimenituma kwamba kuna haja ya kufanya taifa kuwa kitu kimoja.

‘Wote tuzungumze lugha moja’ ili taifa liwe moja ni lazima kuwe na maridhiano sisi vyama vya siasa tunaowakilisha vyama siasa hivyo nimeona ni vyema kwanza kuzungumza na vyama vya siasa,” amesema.

Dk. Samia amekipongeza kikosi kazi kwa kazi nzuri waliyofanya na hivyo mapendekezo waliyotoa yatafanyiwa kazi ili kujenga taifa moja.

“Mbali ya kuwepo kwa vuta ni kuvute na kufanyika kwa mikutano si chini ya mara sita ama saba na CHADEMA lakini sasa tunakwenda boti moja, ndio faida ya kukaa meza moja, kwenye mazungumzo amani haikoseni na ndio maana vyoma vyote 19 vipo hapa,” amesema.

The post Sasa ruksa kufanya mikutano ya hadhara- Rais Samia appeared first on soka letu.

Via soka letu https://ift.tt/QmeZ9fS

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT