Skip to main content

Halotel Tanznaia yakabidhi ari jipya la Promosheni ya 7 Bang Bang

Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital

Kampuni ya Mawasiliano ya simu za mkononi ya Halotel Tanzania PLC imekabidhi zawadi ya gari kwa mshindi aina ya IST mpya katika droo ya mwisho ya Promosheni ya wateja iliyofahamika kama 7 bang bang

Promosheni hiyo iliyoendeshwa kwa muda wa wiki 10, iliwapatia fursa mbalimbali wateja wote wa Halotel waliokuwa wakitumia Mtandao wa Halotel kwa muda wa miaka saba ya utoaji huduma bora za Mawasiliano hapa nchini.

Aidha, Tangu kuanza kwa Promosheni hiyo ya bahati nasibu, zaidi ya washindi 140 wameweza kujishindia zawadi mbalimbali zikiwamo vocha, yenye thamani mpaka 100,000, simu janja aina ya Samsung Galaxy A53 na A73, Televishen janja za nchi 50.

Akizungumza leo Januari 5, 2023 wakati wa hafla ya makabidhiano ya gari hilo, Mkurugenzi wa Biashara wa Halotel, Abdallah Salum, amesema kuwa tuna mshindi aliyebahatika kujishindia gari jipya kwa kushiriki katika shindano hili ambapo ni vema zawadi hii kukabidhiwa katika kipindi hiki cha kumalizia msimu wa siku kuu pamoja na kutoa shukrani kwa wateja wetu wanaotumia Mtandao wa Halotel sambamba na kuadhimisha miaka Saba ya utoaji wa huduma hapa nchini .

“Leo tunayo furaha kwa kumkabidhi mshindi wetu amabaye ni mshindi Mkuu wa gari jipya aina ya IST katika droo kubwa ya mwisho ya Promosheni hii ya 7bang bang ambapo Sholastica Haule ndio ameibuka mshindi wa shindano hili.

“Napenda kukupa pongezi unapochukua gari lako na ninakuasa kutumia zawadi hii katika kupiga hatua zaidi kimaisha na isiwe mwisho wa jitihada zako,” amesema Salum.

Aidha, ametumia fursa hii kuwahimiza wateja wa Halotel waendelee kutumia Mtandao huu ambao unaendelea kuwa na ubunifu ili kuhakikisha kila mteja anafurahia huduma za Mawasiliano kwa ubora wa wa hali ya juu.

Kwa upande wa Sholastica Haule , ameishukuru Kampuni ya Halotel na kuwasihi wateja waendelee kutumia Mtandao huo na kushiriki katika Promosheni zinazotolewa na Kampuni ya Halotel ili waweze kujishindia zawadi mbalimbali.

Sambamba na tukio hilo la kukabidhi gari, Kampuni ya Halotel imetumia fursa hiyo kuzindua duka jipya la kisasa linalopatikana Palm Village Mall iliyopo Mikocheni Dar es Salaam ambapo wateja wa Halotel watapata huduma zote hapo.

Aidha, duka hilo liliboreshwa kwa njia ya Kidijital na litatoa huduma zote zitakazojumuisha usajiki wa laini kutoka 3G kwenda 4G, huduma za vocha ,uthibitisho wa namba za simu, huduma za Halopesa, bidhaa za Halotel Kama router na huduma za ziada na baada ya malipo.

Naye Mkurugenzi wa Mauzo wa Kanda ya Dar es Salaam, Rodrigue Paul amesema kuwa uzinduzi wa duka hilo unaenda sambamba na mkakati wa Halotel kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja na kutimiza ahadi yake kuwapatia wateja fursa ya kupata bidhaa na huduma kwa ukaribu na rahisi.

“Tunapenda kuwakaribisha wateja na watanzania wote kwa ujumla katika duka letu hapa Palm Village Mall waweze kujipatia na kufurahia huduma Bora,” amesema Rodrigue

The post Halotel Tanznaia yakabidhi ari jipya la Promosheni ya 7 Bang Bang appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/65376/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT