Skip to main content

OSCAR OSCAR:- HAWA YANGA BADO NI WAPIGA RAMLI TU ….

OSCAR OSCAR:- HAWA YANGA BADO NI WAPIGA RAMLI TU …. | Soka La Bongo

Oscar Oscra/MwanaSpoti

Wachezaji wa kigeni nchini huwa hawaachwi moja kwa moja. Usishangae siku Saido Ntibazonkiza akirudi tena Yanga. Usishangae Bernard Morrison akirudi tena Simba siku moja.

Mzunguko mdogo wa wachezaji na viongozi ndio chanzo cha haya. Umewahi kujiuliza kwa nini Real Madrid wanalitawala soka la Ulaya muda mrefu sasa? Na pia kuwaacha wengine mbali sana kwenye mataji ya UEFA?

Haya ya Real Madrid yameletwa na uwepo wa fedha chini ya rais wa klabu hiyo, Florentino Perez pamoja na ushawishi wake. Kutokana na ushawishi wa huyu mzee ndio maana unaona wachezaji wengi wazuri wanatamani kucheza Real Madrid.

Angalia pale Manchester United wana pesa ila wanakosa ushawishi wa mtu kama Perez. Ndiyo maana usajili wao bado haujawalipa tangu kuondoka kwa Sir Alex Ferguson.

Wakati mwingine unaweza ukasema pesa haiwezi kukupa kila kitu, ila hiyo pesa kwa asilimia kubwa ndiyo itakupa kile ambacho unakitamani. Ukirudi hapa Afrika katika michuano ya Ligi ya Mabingwa utaona klabu za Ukanda wa Afrika Kaskazini ndizo watawala wa mashindano hayo.

Waangalie Al Ahly ya Misri, hawa jamaa wamechukua mara 10 Ligi ya Mabingwa Afrika. Unajua sababu ni nini? Jibu ni uwekezaji ambao unahitaji pesa.

TP Mazembe kuna wakati nao walikuwa na matumizi makubwa ya pesa ndio maana unawaona hadi sasa wameshinda mataji matano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Soka limekuwa ni biashara kubwa ndio maana unaona hapa kwetu tumekuwa tukisajili wachezaji wa kigeni, ila wale wengi wamemaliza mikatabao au wameachwa walikotoka.

Kila mwana Simba ukikutana nae kijiweni muulize, unataka Luis Miquissone arejee katika timu yako? Atakwambia ndiyo! Ila kwa sasa Miquissone amepanda thamani sio yule ambaye aliondoka Simba mwaka jana.

Hii inaonyesha kuwa bado klabu hasa hizi kongwe za Simba na Yanga hazina msuli wa kusajili mchezaji wa kigeni ambaye yupo ndani ya mkataba. Miquissone ametuonyesha uhalisia wetu.

Kwa sasa Miquissone ana mkataba wa miaka mitatu na mshahara wake ni zaidi ya Sh110 milioni. Je hawa Simba ambao wanahusishwa kumrejesha wako tayari kulipa hiyo fedha? Jibu unalo kichwani.

Inaweza ikatokea nchini klabu moja ikashinda taji la michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sababu tu mpira wakati mwingine una matokeo ya kikatili, ila hilo jambo haliwezi kuwa na mwendelezo kama hakutakuwa na wachezaji wenye ubora mkubwa ambao wanapatikana kwa fedha nyingi.

Leicester City waliwahi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England (EPL) msimu wa 2015/2016 ila kwa sasa unawaona wanachopitia pale England. Ni wachovu tu. Ni watu wanaowaza kukwepa kushuka daraja kila msimu.

Ili Simba na Yanga zishindane na miamba mikubwa Afrika katika soka ni lazima ziwe na pesa ya kutosha ambayo itazisaidia kusajili wachezaji wenye thamani kama hawa kina Miquissone.

Twendeni taratibu huko mbeleni tunaweza kufika nchi ya ahadi katika soka la Afrika kwa upande wa klabu. Ukitazama makundi ya michuano ya klabu Afrika utagundua kuwa timu zetu zimepangwa na timu ambazo kimsingi hazitishi kabisa, lakini bado hatuna uhakika wa kufuzu.

Simba miaka mitano iliyopita walikuwa na kikosi cha maangalizi lakini hakipo kwa sasa. Yanga wameanza kujenga timu. Wamekuwa bora soka la ndani, lakini kimataifa bado ni wapiga ramli. Hakuna uhakika. Wanasuasua tu.

Ndiyo maana basi tunasajili wachezaji mtumba. Ndiyo maana basi tunasajili wachezaji wengi wenye umri mkubwa. Uzuri wa ligi yetu ya ndani ina maajabu kidogo. Wachezaji wakubwa ndiyo mastaa wa timu zetu.

Ni mara chache sana kuona mchezaji mwenye umri mdogo anakuwa supastaa Bongo. Mchezaji mwenye miaka zaidi ya 30 ni rahisi tu kuwa mchezaji bora wa ligi mwishoni mwa msimu.

Mchezaji mwenye miaka 30 ni rahisi tu kuwa mfungaji bora. Linapokuja suala la kimataifa, timu zetu ni vibonde. Linapokuja suala la michuano ya kimataifa timu zetu ni mchekea. Bado usajili wetu ni wa kutambiana tu sisi kwa sisi.

The post OSCAR OSCAR:- HAWA YANGA BADO NI WAPIGA RAMLI TU …. appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/65179/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT