Skip to main content

MGUNDA : YANGA KUFUNGWA KUMETUAMSHIA ARI YA UBINGWA…

MGUNDA : YANGA KUFUNGWA KUMETUAMSHIA ARI YA UBINGWA… | Soka La Bongo

Nyota wa Simba walirejea mazoezini kwa siku mbili na jana walitua  Tanga kwa mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union, huku kocha Juma Mgunda akizungumzia matokeo ya mechi yao na Polisi na kupasuka kwa Yanga mbele ya Ihefu yameamsha ari mpya ya ubingwa.

Simba ilishinda mabao 3-1 ugenini dhidi ya Polisi mechi iliyopigwa mjini Moshi, huku Yanga ikipasuka ugenini mbele ya Ihefu jijini Mbeya na Mgunda alisema matokeo hayo yameirudisha kikosi hicho katika mbio za ubingwa tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Simba inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 31, moja pungufu na ilizonazo Yanga na Azam zilizopo juu yake na Mgunda alisema malengo makubwa kwa timu hiyo ni kukomaa na michezo iliyopo mbele ili kupata ushindi mingi ili kupunguza umbali wa pointi dhidi ya vinara Yanga iliyodondosha pointi.

Alisema ukiangalia matokeo dhidi ya Mbeya City kuna baadhi hata mashabiki walikuwa wameiona Simba imeondoka kwenye mbio za ubingwa, ila kuifunga Polisi na kupoteza kwa Yanga kumebadilisha upepo na sasa wanajipanga kuhakikisha wanafanya kweli hasa katika duru la pili.

“Kutokana na mwenendo wa ligi ulivyo umbali wa pointi walizotuacha Yanga na Azam na hali ya morali kwa wachezaji itaongezeka na tutapambana zaidi kupata matokeo mazuri,” alisema Mgunda na kuongeza;

“Tuna kazi kubwa ya kufanya pamoja na wachezaji, kwani ushindani wa ligi umekuwa mkubwa kila mechi imekuwa ngumu ila tunahitaji kushinda mfululizo kwani bila ya kufanya hivyo malengo ya kutwaa ubingwa hayataweza kutimia.”

“Niwapongeze wachezaji wangu licha ya ugumu wa ratiba kucheza mechi kila baada ya siku tatu wamekuwa wakipambana na kuhakikisha Simba inapata matokeo mazuri kwani bila ya ubora wao kazi itakuwa ngumu kwa upande wangu. Nimekaa nao kuzungumza nao kila mmoja kufahamu tunatakiwa kupambana kadri ambavyo inawezekana kila mmoja kutimiza majukumu ili kufikia malengo.”

Simba iliondoka jana kwa ajili ya mechi hiyo dhidi ya Wagosi itakayopigwa kesho Jumamosi, jijini Tanga, huku rekodi zikiwabeba mbele ya wenyeji wao kila wanapokuta iwe ugenini ama nyumbani.

The post MGUNDA : YANGA KUFUNGWA KUMETUAMSHIA ARI YA UBINGWA… appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/63886/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT