Skip to main content

KIUNGO MGUMU SIMBA KUIBUKIA GEITA GOLD

JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa atamtumia kiungo wake mgumu kwenye mechi za ligi kwa kuwa adhabu yake itakuwa imegota mwisho.

Kanoute alionyeshwa kadi mbili za njano mbele ya Coastal Union, Desemba 3,2022 ubao uliposoma Coastal Union 0-3 Simba ile ya kwanza alionyeshwa dakika ya 40 na ya pili alionyeshwa dakika ya 90.

Mgunda amesema:-“Atakosa mchezo mmoja ile ni adhabu ambayo ameipata na ukweli ni kwamba Kanoute ni mchezaji wangu muhimu tutamkosa kwenye mchezo mmoja.

“Tutamkosa kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hivyo nina amini kwamba atarejea kwenye mechi zetu za ligi kuendelea kutimiza majukumu yake.

“Tumemaliza mzunguko wa kwanza na sasa hesabu ni kwenye mzunguko wetu wa pili unaona vijana wanacheza kwa kujituma na uwepo wa mashabiki unatufanya tunaendelea kupata matokeo,” alisema Mgunda.

Ataukosa mchezo dhidi ya Eagle ambao ni wa Kombe la Shirikisho raundi ya Pili unaotarajiwa kuchezwa kati ya Desemba 9/11 ataibuka kwenye mchezo wa ligi dhidi ya  Geita Gold, Desemba 18, Uwanja wa Nyankumbu.

The post KIUNGO MGUMU SIMBA KUIBUKIA GEITA GOLD appeared first on Saleh Jembe.

The post KIUNGO MGUMU SIMBA KUIBUKIA GEITA GOLD appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/64302/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT