Skip to main content

Dk. Mpango: Viongozi wanachangia uharibifu wa mazingira

na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

MAKAMU wa Rais, Dk. Philip Mpango amesema, kuna baadhi ya viongozi kwa maslahi yao binafsi wanachangia katika uharibifu wa mazingira.

Dk. Mpango ametoa kauli hiyo Desemba 19, 2022, Iringa katika Kongamano la Wahariri na Wadau wa Uhifadhi, Mazingira na Utunzaji wa Vyanzo vya Maji.

“Wapo baadhi ya viongozi kwa maslahi binafsi, wanachangia sana kwenye uharibifu wa mazingira.

“Siamini wakulima wetu masikini, wafugaji kwamba ndio wanaoharibu mazingira. Lazima tunusuru mito yetu yote hasa mito ya kimkakati kama Ruaha, viongozi wa namna hii hawatufai,” amesema Dk. Mpango.

Katika kongamano hilo amesema, mwaka 1980 uharibifu wa mazingira ulifanywa kwa asilimia 42; mwaka 1980 asilimia 50 na mwaka 2012 uharibifu ulikuwa kwa asilimia
68.

Habibu Mchange

Kwenye kongamano hilo, Deodatus Balile, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ameishauri serikali kuchukua hatua ya kuiondoa Ranchi ya Usangu ambayo ipo ndani ya bonde oevu linalolisha maji Mto Ruaha Mkuu sambamba na kujenga tuta eneo la Ngiliamu ili kuunusuru mto na ukame.

“Sisi tunafanya habari za uchunguzi na tumebaini Ranchi ya Usangu inamilikiwa na familia 12, wamo majaji, wamo wabunge, wamo mawaziri na leo nitakukabidhi majina.

“Ranchi hii ilifutwa na GN No. 28 lakini kamati ya mawaziri wanane iliamua kuiacha,” amesema Balile.

Habibu Mchange ambaye ni Mwenyekiti wa MECIRA amesema, leo ni siku ya 130 Mto Ruaha hautiririshi maji.

“Leo Mto Ruaha Mkuu umefikisha siku 130 bila kutiririsha maji, na ukienda hifadhini utasikitika kuona viboko wanagombania mchanga na si maji kutokana na uharibifu wa mazingira, amesema Mchange.

The post Dk. Mpango: Viongozi wanachangia uharibifu wa mazingira appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/65041/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT