Ubalozi wa China watoa msaada wa vifaa vya matibabu kwa hospitali ya Tunisia Ubalozi wa China nchini Tunisia Jumatano umetoa v…
Ubalozi wa China watoa msaada wa vifaa vya matibabu kwa hospitali ya Tunisia
Ubalozi wa China nchini Tunisia Jumatano umetoa vifaa vya matibabu kwa hospitali ya Mkoa wa Gafsa, kusini mwa Tunisia.
Balozi wa China nchini Tunisia Zhang Jianguo na wafanyakazi wa ubalozi huo walitoa msaada huo walipotembelea hospitali ya mkoa ya Houcine Bouzaienne iliyoko eneo hilo. Vilevile wametoa pesa taslimu kwa hospitali hiyo kununua vifaa vya matibabu vinavyohitajika haraka.
Gavana wa Gafsa Abdelhalim Hamdi ameishukuru China kwa msaada wake, na kuahidi kuzidi kuimarisha na kuendeleza ushirikiano wa kirafiki na China.
Balozi Zhang wa China amesisitiza haja ya kukuza ushirikiano wa matibabu kati ya China na Tunisia na kuwakaribisha wafanyakazi wa afya wa Tunisia kutembelea na kujifunza nchini China.
The post Ubalozi wa China watoa msaada wa vifaa vya matibabu kwa hospitali ya Tunisia Ubalozi wa China nchini Tunisia Jumatano umetoa v… appeared first on soka letu.
source https://mjombazecoder.website/61444/
Comments
Post a Comment