Rooney Amchana Ronaldo kwa Mara Nyingine, Amtaka Ajitathmini Upya
Wayne Rooney na Cristiano Ronaldo wamecheza pamoja Old Trafford
MFUNGAJI Bora wa muda wote wa Manchester United Wayne Rooney ameibuka kwa mara nyingine na ksema kuwa nyota wa Manchester United Cristiano Ronaldo anapaswa kujitathmini na kuendelea kufanya mazoezi kwa nguvu kujiweka sawa pale Kocha atakapomhitaji basi awe msaada kwa timu.
Rooney amebainisha kuwa vitendo vya utovu wa nidhamu alivyovionesha nyota huyo kwa siku za hivi karibuni havivumiliki ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo na visingeweza kuvumilika enzi wanacheza pamoja Old Trafford.
Wayne Rooney amesema vitendo vya utovu wa nidhamu alivyofanya Ronaldo havikubaliki ndani ya klabu ya Manchester United
Ikumbukwe Ronaldo aligoma kuingia uwanjani katika dakika za majeruhi kwenye mchezo wa Ligi Kuu nchini Uingereza dhidi ya Totenham Hotspurs hivi karibuni na kuzua taharuki baada ya kuamua kuondoka kabisa uwanjani kabla ya mchezo huo kumalizika.
“Kwa Cristiano ni shusha kichwa chini fanya mazoezi na kuwa tayari kucheza pale Kocha anapokuhitaji, kama atafanya hivyo basi atakuwa hazina kubwa lakini kama hatafanya hivyo basi atakuwa ni mtu mharibifu na asiyehitajika.
Toa comment
The post Rooney Amchana Ronaldo kwa Mara Nyingine, Amtaka Ajitathmini Upya appeared first on soka letu.
source https://mjombazecoder.website/59989/





Comments
Post a Comment