Mwanaharakati aliyevamia Uwanja wakati wa mechi kati ya Ureno na Uruguay hatochukuliwa hatua za kisheria bali anafukuzwa Qatar. …
Mwanaharakati aliyevamia Uwanja wakati wa mechi kati ya Ureno na Uruguay hatochukuliwa hatua za kisheria bali anafukuzwa Qatar.
Mario Ferri (35) aliingia kwenye Uwanja wa Lusail Jumatatu huku akipunga bendera yenye rangi za upinde wa mvua akiwa amevaa tisheti ambayo kwa mbele iliandikwa “Okoa Ukraine” na kwa nyuma “Heshima kwa wanawake wa Iran”.
Alikimbizwa na kukamatwa na maafisa wa Usalama.
Kwa mujibu wa Kamati Kuu ya Kombe la Dunia 2022 kibali chake cha kuingia Qatar kimefutwa, na amefungiwa kutohudhuria mechi zingine katika Mashindano haya.
Taarifa kutoka Italia zinasema Mario ni mwanasoka ambaye amekuwa akichezea timu mbalimbali.
Ana historia ya kuvamia viwanja kwenye mechi, alifanya hivyo mwaka 2014 kwenye Kombe la Dunia nchini Brazil, wakati wa mechi kati ya Ubelgiji na Marekani na mwaka 2017 wakati Napoli ikicheza na Juventus.
#KitengeSports

The post Mwanaharakati aliyevamia Uwanja wakati wa mechi kati ya Ureno na Uruguay hatochukuliwa hatua za kisheria bali anafukuzwa Qatar.
… appeared first on soka letu.
source https://mjombazecoder.website/63592/
Comments
Post a Comment