Muigizaji aliyeshiriki kwenye filamu maarufu za “Die Hard” na “Top Gun” Clarence Gilyard (66) amefariki Dunia. Kifo chake kimet…
Muigizaji aliyeshiriki kwenye filamu maarufu za “Die Hard” na “Top Gun” Clarence Gilyard (66) amefariki Dunia.
Kifo chake kimetangazwa na Chuo Kikuu cha Nevada ambako hadi hivi karibuni alikuwa akifanya kazi kama Profesa wa filamu na uigizaji.
Aliigiza kwenye filamu mbalimbali ikiwemo Die Hard (1988) akishirikiana na Bruce Willis na Alan Rickman, pia aliigiza Top Gun (1986) akiwa na Tom Cruise.
Ameifanyia kazi sekta ya filamu na televisheni ya nchini Marekani kwa miaka zaidi ya 30 akiigiza, kuandika , kusimamia filamu na akifundisha uigizaji Chuo Kikuu.
#KitengeUpdates

The post Muigizaji aliyeshiriki kwenye filamu maarufu za “Die Hard” na “Top Gun” Clarence Gilyard (66) amefariki Dunia. Kifo chake kimet… appeared first on soka letu.
Via soka letu https://ift.tt/AqnmuEs
Comments
Post a Comment