Skip to main content

Mpole, Geita Gold Wavutana Baada ya Kutoonekana kwa Muda Kikosini



Mpole, Geita Gold Wavutana Baada ya Kutoonekana kwa Muda Kikosini

Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, George Mpole.

MFUNGAJI Bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, George Mpole, ameibuka na kufunguka mengi makubwa yanayomuhusu mara baada ya kutoonekana kwa muda kikosini hapo.

Hiyo ikiwa siku ni siku chache zimepita tangu uongozi utoe taarifa za mshambuliaji huyo kutoweka kambini wakati timu hiyo ikiendelea kucheza michezo ya Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Spoti Xtra, Mpole alisema hayupo katika timu hiyo, kutokana na kuuguza majeraha ambayo hivi sasa yanaendelea vizuri baada ya kutumia gharama zake mwenyewe.

Mpole alisema anawashukuru wale ambao wanajali uwezo wake, hasa Watanzania wanaompenda na kuona umuhimu wake kwa kumpigia simu wakimtakia heri akiwa anaendelea kujiuguza.

Aliongeza kuwa anashangazwa na uongozi wake kugomea kumlipa mshahara wake, kwa sababu ya kutokuwa na timu wakiwa wanafahamu kabisa yeye ni majeruhi na daktari ana taarifa zake.

“Viongozi wanaosema Mpole hayupo kwenye timu ndio haohao waliosema nisiwekewe mshahara kwa sababu sitaki kucheza, wakati kiuhalisia mimi nina majeraha.

“Mimi sijalipwa mshahara na timu ambayo nimepata majeraha nikiwa naipambania ili ipate matokeo ugenini, sijalipwa mshahara kwa sababu zisizo za msingi, daktari wa timu taarifa zangu anazo. Kuna wachezaji wengine wapo nyumbani zaidi ya miezi miwili na wanalipwa, lakini mimi nimeumia siku chache siwekewi mshahara.

“Lakini nashukuru kwa sasa naendelea vizuri, watu wananipa ushirikiano na tayari nimeanza mazoezi, muda si mrefu nitarudi,” alisema Mpole.

Wakati Mpole akiyasema hayo, uongozi wa Geita Gold umeibuka na kukanusha vikali tuhuma hizo kutoka kwa mshambuliaji wao.

Akizungumza na SpotiXtra, Mkuu wa Idara ya Habari wa Geita Gold, Hemed Kivuyo, alisema: “Uongozi haukuwa na taarifa zozote kuhusiana na Mpole kuwa na majeraha.

“Nakumbuka tulipokuwa Tanga kucheza dhidi ya Coastal Union, baada ya mchezo huo Mpole aliomba ruhusa ya kwenda Dar, akasema ataungana na timu kuelekea mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shooting ambao ulifanyika jijini Dar.

“Kweli tulivyofika Dar aliungana na timu mazoezini, lakini kwa muongozo wa Kocha Mkuu (Fred Felix Minziro) alisema atatumia wachezaji ambao walicheza kwenye mechi iliyopita dhidi ya Namungo.

“George Mpole ni mchezaji wetu na kikubwa anachotakiwa kufanya ni kuzungumza na uongozi ili kumaliza tofauti au sintofahamu inayoendelea na hatimaye arejee ndani ya timu.”

Mara ya mwisho Mpole kuonekana uwanjani ilikuwa Oktoba 13, mwaka huu katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ambapo Geita Gold na Coastal Union zilishindwa kufungana katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

STORI NA WILBERT MOLANDI NA NAILA SHOMARI







Toa comment

The post Mpole, Geita Gold Wavutana Baada ya Kutoonekana kwa Muda Kikosini appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/59852/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT