LUSINDE AMTAKA DK. BASHIRU AJIUZULU MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo…
LUSINDE AMTAKA DK. BASHIRU AJIUZULU
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mvumi Livingston Lusinde amemtaka aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk Bashiru Ally Kujizulu nafasi yake ubunge.
Lusinde ameyasema hayo Leo jijini Dodoma baada ya kukerwa na kauli ya Dk. Bashiru alizotoa Mkoani Morogoro akiwa katika kikao na wakulima.
Amesema Balozi Dk.Bashiru jimbo lake ni Ikulu kwasababu ameteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kama anaona hawezi kufanya kazi na uongozi uliopo madarakani ni vyema akaachia ngazi na nafasi yake ikachukuliwa na mtu mwingine,
“Bashiru amekuwa Katibu Mkuu wa Chama, Katibu Mkuu Kiongozi na balozi, ana mambo mengi ya nchi hii ambayo anayajua, hivyo kuzungumza maneno yale siyo maneno yanayoweza kunyamaziwa kimya.”
“Jimbo la Balozi Dk.Bashiru ni ikulu kwasababu ndio imemteua, si kumbuki kama kuna siku aliwahi kumshukuru Rais Samia kwa kumteua, kwasababu anajisikia vibaya akisikia watu wanasema Rais Samia anaupiga mwingi anatakiwa aachie ngazi ili ateuliwe Mbunge mwingine ambaye atapendezwa na kile kinachofanywa na serikali ya awamu ya sita.” amesema
Lusinde amesema Balozi Dk.Bashiru akiwa Katibu Mkuu wa CCM aliwafundisha kuimba mapambio ya kusifu na walifanya hivyo sasa kwanini wakati huu inamkera.
#KitengeUpdates

The post LUSINDE AMTAKA DK. BASHIRU AJIUZULU MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo… appeared first on soka letu.
Via soka letu https://ift.tt/rPm9tRy
Comments
Post a Comment