Skip to main content

KISA UCHAGUZI …KADUGUDA ALIAMSHA SIMBA SC…AANIKA SAFARI YA BARBARA QATAR..

KISA UCHAGUZI …KADUGUDA ALIAMSHA SIMBA SC…AANIKA SAFARI YA BARBARA QATAR.. | Soka La Bongo

Klabu ya Simba SC ipo tayari kufanya Uchaguzi Mkuu wa Viongozi upande wa Wanachama ambao wataamua nani atakwenda kuwawakilisha kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu hiyo.

Simba SC kwa sasa inongozwa na Mwenyekiti Multaza Mangungu ambaye alichaguliwa kuziba nafasi ilioachwa wazi na Swedi Nkwabi ambaye aliamua kujiuzulu mwaka mmoja, baada ya kuchaguliwa na Wanachama.

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ambaye ni sehemu ya viongozi waliopatikana kupitia Uchaguzi Mkuu wa miaka minne iliyopita, Mwina Seif Mohamed Kaduguda, amethibitisha kuwa Mchakato Uchaguzi Mkuu wa Simba SC upo tayari na wakati wowote utatangazwa hadharani na Afisa Mtendaji Mkuu Barbara Gonzales.

Kaduguda ameweka wazi harakati hizo za Uchaguzi alipohojiwa na Kituo cha Radio cha EFM, huku akisema hakutakua na danadana.

“Uchaguzi wa Simba SC hauna danadana. Tarehe ya Uchaguzi imeshapangwa na Mtendaji Mkuu wa klabu Barbara Gonzales atakuja kuutangaza. Mimi sio msemaji katika hili, lakini juwa Uchaguzi uko na utakuja kutangazwa.”

“Kwa sasa Barbara yuko Qatar kwenye Fainali za Kombe la Dunia, amekwenda huko kwa ajili ya kujifunza vitu mbalimbali vya kuifanya Simba SC izidi kwenda juu. Uzuri Wanasimba hawana tatizo na Uchaguzi wao,” amesema Mwina Kaduguda

Tangu Simba SC ilipoingia katika Mfumo wa Mabadiliko ya Kiutendaji, imekua ikiendeshwa kwa mfumo wa Uongozi kutoka kwa Mwekezaji na sehemu nyingine inatoka kwa Wanachama, ili kuunda Bodi ya Wakurugenzi ambayo hufanya maamuzi ya Kimaendeleo ya Klabu hiyo.

The post KISA UCHAGUZI …KADUGUDA ALIAMSHA SIMBA SC…AANIKA SAFARI YA BARBARA QATAR.. appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/62590/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT