Skip to main content

KISA SIMBA…MBEYA CITY TUMBO JOTO….HAWAJUI WAACHE KIPI AU WACHUKUE KIPI…

KISA SIMBA…MBEYA CITY TUMBO JOTO….HAWAJUI WAACHE KIPI AU WACHUKUE KIPI… | Soka La Bongo

Wakati Simba SC ikiwasili salama jijini Mbeya tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi Mbeya City, Wenyeji wametangaza kujihami kutokana na matokeo ya sare yanayowaandama.

Simba SC, leo Jumatano (Novemba 23) itakuwa Mgeni wa mchezo huo katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokione jijini Mbeya kuanza mishale ya saa kumi jioni.

Kocha Msaidizi wa Mbeya City Anthony Mwamlima amesema matokeo ya sare katika michezo ya nyuma wakiwa nyumbani yamewahuzunisha, lakini amewaahidi Mashabiki wao wanayafanyia kazi na kesho watakuwa tofauti.

Amesema wanakwenda kucheza na timu yenye uzoefu mkubwa katika Michezo ya Ligi Kuu na ile ya Kimataifa, hivyo wamejipanga kuikabili kwa hali zote, ili kuwafurahisha Mashabiki wao kwa matokeo yatakayowapa matokeo mazuri.

“Hatuna imani na haya matokeo ya sare tunayoyapata, Ligi ni ngumu na inatupasa kulinda nafasi yetu lakini unapopata sare mfululizo nyumbani haipendezi japo ni afadhali kuliko kupoteza.”

“Tunakwenda kukutana na Simba SC katika mchezo ambao tunauangalia kwa jicho la tatu, kwa sababu tunakwenda kukutana na timu kubwa ambayo ina uzoefu wa kutosha, na inacheza michezo ya Kimataifa, hivyo maandalizi yetu lazima yawe tofauti na tunavyojiandaa siku zote.” amesema Mwamlima

Mbeya City FC inakwenda kukutana na Simba SC ikikumbuka matokeo ya sare ya bila kufungana dhidi ya Geita Gold FC, huku Mnyama akikumbuka matokeo ya furaha mbele ya Ruvu Shooting iliyokubali kubugizwa mabao 4-0 mwishoni mwa Juma lililopita.

The post KISA SIMBA…MBEYA CITY TUMBO JOTO….HAWAJUI WAACHE KIPI AU WACHUKUE KIPI… appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/62594/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT