Skip to main content

KIMEUMANA YANGA….PANGA KUPITA NA MASTAA HAWA 6 WAKUBWA…INJINIA HERSI APIGILIA MSUMARI…

KIMEUMANA YANGA….PANGA KUPITA NA MASTAA HAWA 6 WAKUBWA…INJINIA HERSI APIGILIA MSUMARI… | Soka La Bongo

Kuelekea usajili wa dirisha dogo hapa nchini unaotarajiwa kufunguliwa Desemba 16, 2022 hadi Januari 15, 2023, mastaa 6 wa Yanga wamekalia kuti kavu kutokana na rekodi zao kuwa hafifu uwanjani.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi, jana Jumanne ilipata ushindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji, uliochezwa Uwanja wa Liti, Singida.

Ni Gael Bigirimana, nyota ambaye hajawa kwenye kiwango bora ndani ya Yanga, huku akiwa hana nafasi kikosi cha kwanza kwa kuwa amecheza mechi tano pekee na kuyeyusha dakika 242.

Dickson Ambundo, staa huyu msimu huu hajawa na mwendo mzuri, amecheza mechi nne za ligi na kusepa na dakika 187 akiwa ametoa pasi moja ya bao.

Joyce Lomalisa, licha ya kufanya vizuri kwenye mchezo dhidi ya Singida Big Stars, bado anatajwa kuwa kwenye uangalizi mkubwa wa benchi la ufundi la timu hiyo kuhusu kiwango chake akiwa ametumia dakika 420 na ametoa pasi mbili za mabao.

Heritier Makambo, mshambuliaji huyu akiwa amecheza mechi nne, kasepa na dakika 243, hajafunga bao wala kutoa pasi ya bao na nafasi yake inatajwa kuchukuliwa na mshambuliaji chipukizi Clement Mzize.

Yusuph Athuman na Crispin Ngushi, hawajaonekana kwenye kikosi cha kwanza kwa kile ambacho kilielezwa kuwa hawakuwa fiti.

Timu hiyo imetinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu na imeweka wazi kuwa inahitaji kufika mbali na kuboresha kikosi hicho kwa mujibu wa ripoti ya kocha.

Injinia Hersi Said, Rais wa Yanga, alisema kuwa mpango mkubwa kwenye mechi za kimataifa na zile za ndani ni kufanya vizuri, huku masuala ya maboresho ya kikosi hayo yakisubiri ripoti ya Nabi.

“Tupo kwenye mashindano ya kimataifa ambayo yanahitaji umakini mkubwa, kikubwa kwenye suala la maboresho ya kikosi chetu ni kuwa na wachezaji wazuri ambao watatupatia matokeo chanya, kazi bado inaendelea,” alisema.

The post KIMEUMANA YANGA….PANGA KUPITA NA MASTAA HAWA 6 WAKUBWA…INJINIA HERSI APIGILIA MSUMARI… appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/62592/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT