Skip to main content

Bosi Yanga Ampa Ujanja Nabi Kupindua Matokeo Tunisia Dhidi ya Club Africain



Bosi Yanga Ampa Ujanja Nabi Kupindua Matokeo Tunisia Dhidi ya Club Africain

ALIYEWAHI kuwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, amesema timu hiyo ina kibarua kigumu cha kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, lakini amemtaka Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi nguvu na akili nyingine aziongeze katika Ligi Kuu Bara.

Kauli hiyo aliitoa kabla ya jana Jumatano Yanga kucheza mchezo wa kwanza wa Play-Off katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Club Africain ya Tunisia uliochezwa Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Yanga imeangukia kwenye michuano hiyo baada ya kuondolewa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal ya Sudan.

Akizungumza na Spoti Xtra, Mwakalebela alisema anafahamu jukumu zito walilonalo kimataifa, lakini hiyo haifanyi kusahau michezo ya ligi.

Mwakalebela alisema kama nguvu kubwa ikielekezwa kimataifa, basi upo uwezekano wa kupoteza taji lao la ubingwa wa ligi ambalo wanalitetea msimu huu.

Aliongeza kuwa, Kocha Nabi anatakiwa kufanya maandalizi ya ligi na kimataifa ndani ya wakati mmoja kwa lengo la kutotoka kileleni ambako wamewaondoa watani wao, Simba SC.

“Presha ipo kubwa katika timu hivi sasa, hiyo ni baada ya kuondolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika na kuangukia Shirikisho, hivyo kocha, wachezaji na viongozi wanatakiwa kujiongeza.

“Ninafahamu kwamba hivi sasa Yanga wanataka kuthibitisha ubora wao kwa kufuzu makundi Shirikisho wakitumia nguvu na akili nyingi.

“Hivyo hawatakiwi kufanya hivyo wakajisahau, badala yake kuipa umuhimu michezo ya ligi pia kwa lengo la kutetea ubingwa wetu, kwani Simba wanasubiri tuteleze kidogo ili watupoke ubingwa msimu huu,” alisema Mwakalebela.

STORI: WILBERT MOLANDI







Toa comment

The post Bosi Yanga Ampa Ujanja Nabi Kupindua Matokeo Tunisia Dhidi ya Club Africain appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/59023/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT