Benki Kuu ya Tanzania yataka benki zikopeshe kwa riba asilimia 9 Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema lengo lake ni kuona taasis…
Benki Kuu ya Tanzania yataka benki zikopeshe kwa riba asilimia 9
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema lengo lake ni kuona taasisi za kifedha ikiwemo benki zinatoa mkopo kwa wananchi kwa riba isiyozidi asilimia 9.
Kauli hiyo imetolewa jana na Gavana wa BoT, Profesa Florens Luoga kwenye kongamano la uwasilishaji wa machapisho ya wataalam wa fedha kuelekea mahafali ya kwanza ya Chuo cha Benki Kuu Tanzania yanayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii.
Amesema agizo la Rais Samia Suluhu Hassan alilolitoa kwenye uzinduzi wa jengo la BoT mkoani Mwanza Juni 13, 2021, akiitaka benki hiyo kuhakikisha riba katika taasisi za kifedha ikiwemo mabenki inashushwa, limetekelezwa kwani hadi sasa benki nchini zinatoa mkopo kwa riba ya kati ya asilimia 11 na 13.
The post Benki Kuu ya Tanzania yataka benki zikopeshe kwa riba asilimia 9 Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema lengo lake ni kuona taasis… appeared first on soka letu.
source https://mjombazecoder.website/62775/
Comments
Post a Comment