LEO ni dabi kwenye Uwanja wa Mkapa. Achana na vitu vingine vyote ila rekodi zinaonyesha michezo yao ya Oktoba hakuna aliyeibuka mbabe katika mara 19 zilizokutana tangu Ligi Kuu Bara ilipoasisiwa 1965, Yanga na Simba kila moja imeshinda mara sita huku mara saba zikienda sare. OKTOBA 7, 1979 Simba 3-1 Yanga Simba ilipata bao dakika ya 3 lililofungwa na Nico Njohole kabla ya Yanga kuchomoa kupitia kwa Rashidi Hanzuruni dakika ya 4 huku Mohammed Bakari ‘Tall’ na Abbas Dilunga wakiihakikishia Simba pointi tatu muhimu. OKTOBA 4, 1980 Simba 3-0 Yanga Mabao ya Simba katika mchezo huu yalifungwa na Abdallah Mwinyimkuu dakika ya 29, Thuwein Ally dakika ya 82 na Nico Njohole dakika ya 83. OKTOBA 20, 1990 Yanga 3-1 Simba Katika mchezo huu mabao ya Yanga yalifungwa na Makumbi Juma, Thomas Kipese na Sanifu Lazaro wakati lile la Simba lilifungwa na Edward Chumila. OKTOBA 9, 1991 Yanga 2-0 Simba Yanga iling’ara kwa mabao ya Athumani China pamoja na Abubakar Salum ‘Sure Boy’. OKTOBA 27, 1992 Simba 1-0 Yanga , Simba ilitakata baada ya kushinda bao 1-0 lililofungwa na Damian Kimti. OKTOBA 4, 1995 Simba 2-1 Yanga Simba ilipata mabao yake kupitia Said Mwamba ‘Kizota’ na Mchunga Bakari huku lile la Yanga likifungwa na Mohammed Hussein ‘Mmachinga’. OKTOBA 23, 1996 Yanga 1-0 Simba Katika mchezo huu bao pekee la Yanga liliweka nyavuni na mshambuliaji, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ dakika ya 46. OKTOBA 11, 1997 Yanga 1-1 Simba Mechi hii iliyopigwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Yanga ilipata bao la Sekilojo Chambua kisha George Masatu kuichomolea Simba dakika za majeruhi. OKTOBA 29, 2006 Simba 0-0 Yanga Miamba hii ilishindwa kutambiana katika mchezo huu. OKTOBA 24, 2007 Simba 1-0 Yanga Huu ni mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ambapo bao la Simba lilifungwa na Ulimboka Mwakingwe. OKTOBA 26, 2008 Yanga 1-0 Simba Mechi hii iliyopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Yanga ilifunga bao hilo kupitia kwa Ben Mwalala dakika ya 15 ya mchezo na kupeleka furaha kwa wana Jangwani hao. OKTOBA 31, 2009 Simba 1-0 Yanga Mtanange ulipigwa Uwanja wa Taifa na Simba ilipolipa kisasi kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0, lililowekwa nyavuni na mshambuliaji wake hatari kipindi hicho, Mussa Hassan Mgosi. OKTOBA 16, 2010 Yanga 1-0 Simba Mshambuliaji aliyewika kwa wakati huo, Jerry Tegete alipeleka kilio kwa wana Msimbazi baada ya kufunga bao hilo dakika ya 70. OKTOBA 29, 2011 Yanga 1-0 Simba Bao la Davies Mwape dakika ya 75 ya mchezo lilipeleka furaha kwa mashabiki wa Yanga waliohudhuria mechi hiyo iliyokuwa na msisimko. OKTOBA 3, 2012 Yanga 1-1 Simba Simba ilipata bao la mapema dakika ya 4 tu kupitia kwa Amri Kiemba kabla ya Said Bahanuzi kuisawazishia Yanga dakika ya 65 kwa penalti. OKTOBA 20, 2013 Yanga 3-3 Simba Ni ngumu sana kwa idadi sawa ya mabao katika mechi ya watani wa jadi, Yanga na Simba. Hata hivyo rekodi hiyo iliwekwa katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu msimu wa 2013-2014 uliopigwa Oktoba 20, 2013 Yanga ilifunga mabao matatu kipindi cha kwanza na Simba kujipatia yake kipindi cha pili na mechi kuisha kwa sare ya 3-3. Mabao ya Yanga yalifungwa na Mganda Hamis Kiiza (mawili) na Mrisho Ngassa. Hata hivyo, kipindi cha pili Simba ilisawazisha mabao yote matatu yaliyofungwa na Joseph Owino, Bertram Mwombeki na Gilbert Kaze. OKTOBA 18, 2014 Yanga 0-0 Simba Timu hizi zilishindwa kutambiana baada ya mchezo huu kuisha kwa suluhu. OKTOBA 01, 2016 Yanga 1-1 Simba Katika kipindi cha miaka 10, mchezo huu wa Oktoba Mosi, 2016 unakumbukwa zaidi kutokana na bao la kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya alilofunga katika mechi iliyomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1 . Yanga ikiwa na imani ya kuendeleza ubabe kwa watani wao, kwani ilikuwa imetoka kuinyoa timu hiyo mara mbili kwa mabao 2-0, hasa baada ya kutangulia kupata bao lililozua utata la mshambuliaji wake Amissi Tambwe. Tambwe alifunga bao lililoonekana la kuutengeneza kwa mkono na kusababisha aliyekuwa nahodha wa Simba, Jonas Mkude kuonyeshwa kadi nyekundu. Wakati Yanga ikiamini inaondoka na pointi tatu, Kichuya aliyekuwa moto enzi hizo alipiga mpira wa kona katika dakika dakika 87 ulioenda moja kwa moja wavuni na kuisawazishia Simba bao hilo na matokeo kumalizika kwa sare ya kufungana 1-1. OKTOBA 28, 2017 Yanga 1-1 Simba Simba ilitangulia kupata bao kupitia kwa Shiza Kichuya dakika ya 57 kisha Obrey Chirwa akaisawazishia Yanga dakika ya 60.
The post ZE KICK: Oktoba mwezi dume kwelikweli Kariakoo Dabi appeared first on soka letu.
Via soka letu https://ift.tt/4syz5Jj
Comments
Post a Comment