Skip to main content

Watu milioni 2.8 wapata chanjo ya Uviko Dar

Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

ZAIDI ya watu milioni 2.8 ambao sawa na asilimia 85 wamepatiwa chanjo ya ugonjwa wa uviko 19 katika Mkoa wa Dar es salaam tangu ilipozinduliwa na Rais Samia Suluhu Hasani, Agosti 30, mwaka jana.

Mhariri Mkuu wa Jarida la FAMA, Neville Meena, akielezea jambo kwenye warsha.

Akizungumza kwenye warsha ya majadiliano iliyoandaliwa na internew kuhusu umuhimu wa Chanjo hiyo katika jamii Afisa Afya mkoani hapa, Enezael Ayo, amesema watu wamehamasika kutokana na elimu pamoja ongezeko la vituo vya uchanjaji.

Amesema kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2012, mkoa wa Dar es Salaam ulikuwa na makadirio ya idadi ya watu Milioni 6, ambapo kati yao zaidi ya watu milioni 3.3 ambayo ni asilimia 75, wamefikiwa na Chanjo hiyo.

“Tunaendelea kuhamasisha wananchi waendelee kuchanja kwani chanjo ni salama na Haina madhara Kwa binadamu kama uvumi unavyoelezwa huko mitaani.

“Tegemeo la rasilimali ya nchi Ni watu hivyo Basi hakuna kiongozi wa nchi anayependa watu wake kufariki Kwa sababu ndio rasilimali ya taifa,” amesema Ayo.

Amesema mkoa huu ulilazimika kuongeza vituo maeneo mbalimbali Kwa ajili ya uchanjaji ambapo awali vilikuwa vituo vitatu tu Mpaka Sasa Kuna vituo 318.

Kwa upande wake, Daktari anayejitegemea, Dk. Christina Mdingi, amesema jamii inatakiwa kupuuza baadhi ya viongozi wa dini mbalimbali wanao eneza uvumi kuwa Chanjo hiyo si salama sababu hakuna taarifa ya madhara yatokanayo na uchanjaji.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC), Samson Kamalamo, amesema mafunzo haya yatasaidia Wanahabari kutoa taarifa sahihi Kwa jamii kuhusiana na ugonjwa huo.

“Yote tuliyojifunza hapa tunaenda kuyafanyia kazi, kwa sababu huu ni mwanzo tu tumejiandaa kufanya mikutano mingine pamoja na warsha kwa lengo la kuwafanya wananchi kuwa aware,” anasema Kamalamo.

The post Watu milioni 2.8 wapata chanjo ya Uviko Dar appeared first on soka letu.

Via soka letu https://ift.tt/RXL63uz

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT