Skip to main content

Watu milioni 1.6 wamepata chanjo kamili ya uviko 19 Mwanza

Na Clara Matimo, Mwanza

Jumla ya wananchi milioni 1.6  kati ya milioni 1.8 waliokusudiwa kupata chanjo ya uviko 19 mkoani Mwanza wamepata chanjo kamili ya kujikinga na ugonjwa huo.

Hayo yamebainishwa Oktoba 18, 2022 na Mganga Mkuu wa mkoa huo, Dk. Thomas Rutachunzibwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye kikao cha tathmini ya chanjo ya Uviko 19 na uhuru wa kupata habari kupitia mradi wa Boresha Habari unatekelezwa na Internews kwa ufadhili wa USAID na  fhi360 ambao unaratibiwa na klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza(MPC).

Dk. Rutachunzibwa alisema idadi hiyo ni  mpaka Oktoba 17, 2022  ambayo ni sawa na asilimia 87 ya lengo ambalo ni kuwachanja chanjo hiyo watu milioni 1.8  hadi ifikapo Desemba 2022.

“Hadi sasa bado watu 200000 tunaimani tunaweza kuvuka lengo na mafanikio haya tumeyapata kutokana na nyie waandishi wa habari kwa kuandika habari sahihi kuhusu chanjo ya uviko 19, taarifa na elimu ambazo mnazitoa kuhusu chanjo ya uviko 19  kupitia vyombo vyenu vya habari  zimesaidia sana kuwapa wananchi uelewa na zimewaondolea mitazamo hasi waliokuwa nayo kuhusu chanjo hiyo.

“Lengo la kitaifa ni kuchanja asilimia 70 ya watu wenye sifa ya kupata chanjo hiyo hadi ifikapo Desema 2022 kwa hiyo nawasihi waandishi wa habari endeleeni kuwaelimisha wananchi kupitia vyombo vyenu ili ambao bado hawajapata chanjo hiyo wapate.

Kwa mujibu wa Dk Rutachunzibwa wilaya inayoongoza mkoani humo kwa kuchanja watu wengi ni Ukerewe ambayo imechanja asilimia 89.4  huku wilaya ya Misungwi ikiwa ya mwisho kwa kuchanja asilimia 74.3.

Mwenyekiti wa MPC Edwin Soko akitoa mada kuhusu  jinsi ya kuripoti habari za chanjo ya uviko 19 na uhuru wa vyomba vya habarai aliwasisitiza waandishi wa habari kuhakikisha wanapoandika habari zao hasa za afya zikiwemo zinazohusu ugonjwa wa Uviko 19 kuhakikisha taarifa hizo zinathibitishwa na wataalamu wenye taaluma ya idara hiyo ili wananchi wapate taarifa sahihi.

“Serikali inatutegemea sana waandishi wa habari kuwafikishia taarifa sahihi wananchi wake katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya afya, inapotokea jambo jipya  baadhi ya wananchi huwa na tabia ya kuzusha wakisema mambo ambayo hawana elimu nayo, nyie wenyewe ni mashahidi wakati chanjo ya Uviko 19 ilipoingia nchini wapotoshaji nao waliibuka.

“Wapo waliosema kwamba mtu ukichanja halafu ukaweka balbu eneo ulilochanja inawaka, huo ni uzushi kabisa nia yao ni kurudisha nyuma jitihada za serikali katika kuzuia na kupambana na ugonjwa huo, jamani kwenye hilo kuna ukweli wowote ? Alihoji na kuongeza.

“Sisi wenyewe tulio wengi tumechanja je tukiweka balbu zinawaka? Kwa hiyo tujitahidi kuhakikisha tunawapa taarifa sahihi wananchi ili wasipotoshwe na watu wachache ambao ni wataalamu wa kuzusha,”alisema Soko.

The post Watu milioni 1.6 wamepata chanjo kamili ya uviko 19 Mwanza appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/58103/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT