Skip to main content

Tanzania Yaingia Robo Fainali Kombe la Dunia Chini ya Miaka 17




Tanzania Yaingia Robo Fainali Kombe la Dunia Chini ya Miaka 17

Canada ilitolewa kwenye Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake U-17 Jumanne baada ya kutoka sare ya kwanza na Tanzania 1-1 katika mchezo wake wa mwisho wa raundi ya ufunguzi.

Vijana hao wa Canada hao waliingia kwenye kinyang’anyiro hicho wakihitaji ushindi mbele ya watu 3,728 kwenye Uwanja wa DY Patil.

Amanda Allen aliipatia Canada bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti. Lakini Tanzania hawakurudi nyuma waliendelea na mashambulizi na hatimaye Veronica Mapunda aliisawazishia Serengeti Girls.

Huku wakiwa wanahitaji ushindi, Wacanada walibadilisha mbinu za mchezo na kufanya mashambulizi makali lakini vijana wa Tanzania walisimama imara kwa uthabiti Canada walikosa umaliziaji kwani kunako dakika za lala salama shuti kali la Jade Bordeleau liliishia mikononi mwa kipa wa Tanzania.

Ikijulikana kwa jina la Serengeti Girls, Tanzania inashiriki kwa mara ya kwanza katika hafla ya Kombe la Dunia la FIFA. Na ilishtua dunia Jumamosi kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Ufaransa baada ya kufungwa 4-0 na Japan katika mechi yake ya kwanza.

Canada ilifungua mchezo kwa sare ya 1-1 na Ufaransa kabla ya kulazwa 4-0 na Japan siku ya Jumamosi.

Japan ilifikisha pointi 9 iliifunga Ufaransa 2-0 na kumaliza kileleni mwa kundi hilo. Tanzania pointi nne ilimaliza katika nafasi ya pili huku Canada ikiishia na pointi mbili ikimaliza ya tatu mbele ya Ufaransa yenye pointi moja.

Ufaransa ilishinda michuano hiyo mwaka 2012 huku Japan ikinyanyua kombe hilo mwaka 2014.

Timu mbili za juu katika kila moja ya makundi manne zinatinga robo fainali Japan dhidi ya Uhispania, Colombia dhidi ya Tanzania, Marekani dhidi ya Nigeria, na Brazil dhidi ya Ujerumani.

Uhispania ndio mabingwa watetezi, baada ya kushinda mwaka 2018 wakati Canada ilishika nafasi ya nne. Mashindano ya 2020 yalifutwa kwa sababu ya janga la Corona.







Toa comment

The post Tanzania Yaingia Robo Fainali Kombe la Dunia Chini ya Miaka 17 appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/57953/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT