Skip to main content

Rekodi zambeba Mgunda Msimbazi

NAMBA hazidanganyi! Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na kinachokifanywa na Juma Mgunda, tangu alipokabidhiwa kikosi cha Simba Septemba 7 akimpokea Zoran Maki aliyetimkia Al Ittihad ya Misri. Uteuzi wa Mgunda kutoka Coastal Union awali ulitajwa ni wa kuokoa jahazi la kuisimamia timu kwenye mchezo wa kwanza wa raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nyasa Big Bullets ya Malawi. Kazi aliyoifanya kwenye mchezo huo na mingine imemfanya kuwafunga midomo waliouponda uteuzi wake, kwani namba zinambeba na kuwafunika baadhi ya makocha wa kigeni walioinoa timu hiyo. Licha ya muda mchache Simba imebadilika kiuchezaji tofauti na kipindi cha nyuma licha ya wachezaji kuwa wale wale ambao kandanda lao lilikuwa halivutii licha ya kushinda michezo yake. REKODI TAMU Tangu Mgunda aanze dhidi ya Nyasa Big Bullet ugenini na kushinda 2-0, kisha Simba ikacheza Ligi Kuu Bara na kuvunja mwiko kwa Tanzania Prisons kwa kuwachapa bao 1-0. Iliporudiana na Big Bullets jijini Dar, ikashinda tena 2-0 na timu kufuzu raundi ya kwanza na baadaye ikacheza Ligi Kuu dhidi ya Dodoma Jiji na kushinda mabao 3-0. Baada ya hapo ikaenda kambini visiwani Zanzibara na kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Malindi na kushinda 1-0, kisha kuipasua Kipanga mabao 3-0 na kusafiri hadi Luanda nchini Angola kuvaana na Primeiro de Agosto katika mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza ya Ligi ya Afrika. Kama ilivyofanya kwa Wamalawi, Simba ya Mgunda ikaikandamiza Agosto mabao 3-1 na kufanya iecheze mechi mechi tano za mashindano na mbili za kirafiki kushinda zote na kufunga mabao 15, yakiwamo 11 ya kimashindano na kuruhusu bao moja pekee dhidi ya Agosto. Rekodi hizo zimafanya waliompinga Mgunda kumkubali kiroho safi na mwenyewe amefunguka, katika maisha yake anamwamini na kumtanguliza Mungu ili aweze kufikia malengo na bahati nzuri ndani ya Simba amekutana na wachezaji wenye uwezo na uelewa mkubwa wa kunasa mbinu zake. “Simba ni timu kubwa kila mtu anayeingia kuitumikia lazima ujipange, naamini tutafanya vizuri kwa ushirikiano na wachezaji na viongozi wetu,” anasema nyota huyo wa kimataifa wa zamani wa Tanzania aliyetamba na Coastal Union na kubeba nao ubingwa wa Bara mwaka 1988. Rekodi hizo zimefunika baadhi ya makocha wa kigeni walioajiriwa kwa gharama kubwa Msimbazi wakiwamo waliorodheshwa hapa chini; PABLO FRANCO Licha ya Simba kukosa ubingwa msimu 2021/22 uliotwaliwa na Yanga Kocha Pablo Franco alishindwa kutimiza malengo yake kimkataba ya kuifikisha timu nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika. Simba ilitolewa katika michuano hiyo na Gwaneng Galaxy baada ya kushinda ugenini mabao 2-0 na ilipoteza nyumbani kwa mabao 3-1 na kuangukia kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho ambapo ilifika robo fainali na kutolewa na Orlando Pirates. Kwa upande wa ligi, Pablo naye alipata ushindi wa mechi mbili akishinda 3-1 na 2-1 na kukusanya pointi sita na mabao matano na kufungwa mawili. ZORAN MAKI Huyu kocha aliyedumu kwa muda mfupi zaidi Simba, siku 67, licha ya muda mchache lakini alisifika kwa ukali uliosababisha baadhi ya wachezaji kukosa morali naye. Mechi zilizochezwa chini yake nyingi ni za kirafiki, ikiwamo zile za pre-season nchini Misri kabla ya kwenda Sudan aliposhinda 4-2 dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana na kupasuka 1-0 kwa Al Hilal kisha na iliporudi nchini ilicheza tena kirafiki na Arta Solar 7 na Simba kulala tena 1-0 na katika ligi, Zoran alicheza mechi mbili akiiongoza Simba kushinda 3-0 dhidi ya Geita Gold kisha kuifumua Kagera Sugar kwa mabao 2-0 na hivyo naye kukusanya pointi sita na mabao matano, bila wavu wake kuguswa kabla ya kujiuzulu Septemba 6 wakati timu ikijiandaa kwenda kucheza na KMC iliyosimamiwa na msaidizi wake, Seleman Matola na kumaliza kwa sare ya 2-2. DIDIER GOMES Huyu aliondolewa Simba baada ya kikosi chake kushindwa kutinga nusu fainali Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika. Simba ilitolewa na Kaizer Cheafs ya Afrika Kusini katika hatua ya robo fainali iliyofanya kocha huyo Mfaransa kufungashiwa virago, lakini alama ameiacha ya kuipa timu hiyo taji la msimu 2020/21. Kwa upande wa ligi, Gomes katika mechi mbili za awali alipata pointi nne alishinda 2-1 akatoka 2-2 na kuachwa nyuma na Mgunda ameliyeshinda mbili na na kukusanya pointi sita na mabao manne, bila wavu wake kuguswa. SVEN VANDENBROECK Aliipa Simba mataji ya matatu msimu 2019/20 na msimu 2020/21 akaiacha timu hatua ya makundi na kusepa zake. Licha ya rekodi hiyo, lakini amezidiwa kimahesabu na Mgunda katika mechi zake za kimataifa na za Ligi. Sven ndiye aliyetisha kwenye mechi mbili za awali akiwa na Simba kwani alishinda 4-0 na 2-0 na kuklusanya pointi sita kama Mgunda, lakini akivuna mabao sita na wavu wake kutoguswa kama ilivyo kwa Mgosi. PATRICK AUSSEMS Mbelgiji Patrick Aussems ‘Uchebe’ aliipeleka makundi Simba kwa mara ya kwanza dhidi ya Nkana ya Zambia mabao 3-1 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa. Mbali na kuweka historia hiyo pia aliipa timu hiyo mataji mawili ya Ligi Kuu msimu wa 2018/19 na msimu wa 2019/2020, kuondolewa kwake Simba ilitokana na tabia yake ya kuwapa uhuru zaidi wachezaji. Katika ligi Aussems alishinda mechi mbili za awali za ligi akishinda 1-0, kisha 2-0 na kukusanya pia pointi sita na kufunga mabao matatu bila wavu wake kuguswa kama Mgunda. WASIKIE WADAU Kenny Mwaisabula mchezaji wa zamani sasa ni kocha anasema, mafanikio yanatokana na makocha wazawa hao wageni wanapewa nafasi kubwa bure. “Wampe nafasi ambayo wanapewa wazungu wampe kila kitu, kuanzia mshahara kama ambao wageni wanalipwa waone atakavyoifikisha timu,” “Mfano Israel Mwenda alivyobadilika muone Chama anafanya kila kitu anashambulia, anakaba na kufunga na kuna mabadiliko ya wachezaji wanaonekana kuwa na furahana kocha wao.’’ “Waswahili hatupendani kitendo cha Simba kumpa heshima Mgunda wengine kinawauma lakini nawapongeza sana viongozi ni jambo jema wamefanya tuwaamini wazawa. Kessy Mziray aliyewahi kukinoa kikosi cha Alliance FC anasema, tatizo la Watanzania hawataki kuamini vya kwao wakati vipo vizuri zaidi ya hao wageni. “Binafsi namuona mbali sana Mgunda endapo watamuamini na kumpa timu sina shaka naye hata kidogo anajua namna gani ya timu icheze kwa wakati gani,’’ anasema. Abdallah Kibadeni anasema Simba ilichelewa kumpata Mgunda kwani uwezo wake ni mkubwa na hata mabadiliko ya timu yanaonekana. “Wapo wazawa wengine kama Fredy Felix ‘Minziro’ wana uwezo sana wapewe nafasi lakini kwa Simba hii Mgunda ndiye wa kuandika historia ya kuifikisha timu mbali zaidi ya hao makocha wengine waliopita na yeye ndiye wa kutuokoa wazawa,’’anasema Kibadeni. Kibadeni anasema Seleman Matola anatakiwa kumsaidia vilivyo Mgunda waaminiwe wapewe timu wanaweza kuifikisha mbali timu. WACHEZAJI SHANGWE Baadhi ya wachezaji wa Simba (Majina tunayo) ambao wameonekana kumuelewa Mgunda wakimuhita ‘Father’ na Matola ‘Brother’. “Mgunda ni zaidi ya kocha sisi wachezaji tunamkubali na tunafurahia kufanya nae kazi, ni kama baba ukikosea anakuonya yanaisha maisha yanaendelea tunamuelewa sana,’’kauli ya nyota Simba. Mgunda mbali nakuwanoa Wagosi naSimba amewahi kuitumikia timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ hivyo uzoefu wake ni mkubwa katika soka.

The post Rekodi zambeba Mgunda Msimbazi appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/57581/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT