Skip to main content

NEEMA NYINGINE YANGA YALETWA NA UNICEF

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Watoto Duniani (Unicef) wameingia mkataba wa kufanya kazi na Klabu ya Yanga kwa muda wa miezi sita huku wakiahidi mengi mazuri.

Yanga wameingia mkataba huo hivi karibuni baada ya pande mbili kufikia makubaliano mazuri kati ya shirika hilo na klabu hiyo.

Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said amesema kuwa sababu kubwa ya kuingia mkataba na Unicef ambalo ni shirika la Umoja wa Mataifa ni kutokana na kuwa na mwendelezo mzuri wa kurejesha kwa jamii pamoja na hati safi, ni jukumu lao klabu kuunga mkono juhudi zitakazowezesha kushinda Uviko -19 na Ebola.

“Yanga na Umoja wa Mataifa kupitia Unicef tumeingia makubaliano ya kufanya nao kazi na kwa kuwa sisi ni klabu tunatoa huduma kwa jamii, maslahi ya kwanza ni kuhakikisha afya zao zinaimarika na kuwapa elimu kuhusu kupata chanjo ya Corona pamoja na kuwa na uelewa kuhusu ugonjwa wa Ebola.

“Gharama za mradi zinalipwa na Unicef na kuna ‘fee’ Yanga inalipwa, gharama zinategemea aina ya mradi ambao utafanyika. Kwenye miundombinu kikubwa ni fedha nguvu za wawekezaji zinatufanya kupata fedha Unicef wao ni watu makini na hii inatuongezea uaminifu na tutapata wawekezaji wakubwa zaidi,” amesema Hersi.

Kwa upande wa Fatimata Balandi, mwakilishi kutoka Unicef Tanzania amesema kuwa wanafurahi kufanya kazi na Yanga kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye mapambano dhidi ya Covid 19 na Ebola.

“Tunafurahi kufanya kazi na Yanga kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye mapambano dhidi ya janga la COVID  19 pamoja na Ebola ambapo tunaamini ndani ya miezi sita tutakuwa tumewafikia wengi  na kuwafanya wawe na uelewa kuhusu Ebola na COVID 19,” amesema Fatimata.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa  Jackson Group, Kelvin Twisa alisema kuwa “Yanga inajihusisha zaidi na jamii yetu kuliko timu nyingine yoyote na UNICEF haibagui mshabiki wa timu yeyote ile.

“Yanga wanapotembelea jamii zetu huwa hawabagui mshabiki wa timu nyingine, maana hili sio swala la ushabiki ni swala la kijamii na Kitaifa kwa ujumla na kazi ya kuelemisha Jamii yetu tunayoenda kushirikiana na UNICEF tutahakikisha wapenzi wa mpira na Wananchi wote namna gani wanaweza kujikinga na maradhi haya,” amesema Twisa.

The post NEEMA NYINGINE YANGA YALETWA NA UNICEF appeared first on Saleh Jembe.

The post NEEMA NYINGINE YANGA YALETWA NA UNICEF appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/58036/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT