Skip to main content

Mzamiru atoa siri kubwa

KIUNGO mkabaji wa Simba, Mzamiru Yassin amefunguka siri ya ubora alionao sasa ndani ya timu yake kuwa ni kurudia kutazama mechi alizocheza ili kutambua makosa yake asiyarudie mechi inayofuata. Mzamiru amekuwa chaguo la kwanza chini ya Kaimu kocha mkuu wa Simba, Juma Mgunda tangu amepewa timu hiyo akichukua nafasi ya Zoran Maki aliyetimkia Misri. Akizungumza na Mwanaspoti, Mzamiru alisema hajabahatisha kuingia kikosini moja kwa moja ni juhudi zake binafsi sambamba na kutumia vyema nafasi ambayo amekuwa akipewa huku akikiri kuwa Simba na Yanga ukiaminiwa unatakiwa kuwaaminisha kuwa hawajakosea kumpa nafasi. “Nafurahi kuwa sehemu ya wachezaji wa kikosi cha kwanza haya ni malengo ya kila mchezaji kwenye timu yake kwani wanasajiliwa wachezaji wengi hatuwezi kucheza wote wanaotakiwa kucheza ni 11 tu hivyo juhudi binafsi za mchezaji ndio siri ya kuweza kupata namba,” alisema na kuongeza; “Wachezaji wote waliopo Simba ni bora tunatofautiana namna ya kucheza hivyo kila mchezaji anatakiwa kupambana kumshawishi kocha kwenye uwanja wa mazoezi ili waweze kupata nafasi ya kucheza kama ilivyo kwa upande wangu.” Akizungumzia mchezo kwa ujumla Mzamiru alisema; “Mara zote dabi ni mchezo mgumu kwasababu wachezaji tunacheza kwa presha kubwa kila mchezaji anataka kuonyesha nini alichonacho, tumeyapokea matokeo tunajipanga na michezo mingine iliyobaki.” Simba itaivaa Azam Alhamisi.

The post Mzamiru atoa siri kubwa appeared first on soka letu.

Via soka letu https://ift.tt/CxOYcNQ

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT