Skip to main content

MPANGO WA AZAM FC, KIPANGA KIMATAIFA IMEGOMA

MPANGO wa Azam FC kwenye mechi za kimataifa umegotea Uwanja wa Azam Complex licha ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Al Khadar ya Libya.

Timu hiyo imeondolewa kwenye Kombe la Shirikisho kwa jumla ya mabao 3-2 kwa kuwa mchezo wa kwanza uliochezwa ugenini Azam FC ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-0 na jana ilikuwa inahitaji ushindi wa mabao 4-0 ili kusonga mbele kimataifa.

Bao la mapema la Idris Mbombo dakika ya 28 liliwafanya waende mapumziko wakiwa mbele kwa bao hilo na kipindi cha pili nyota wa Al Akhadar Ededen Essien alijifunga dakika ya 59 kwenye harakati za kuokoa pigo la Ayoub Lyanga.

Matajiri hao wa Dar sasa wanajipanga kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la FA baada ya kumaliza mwendo kwenye anga za kimataifa kwa msimu wa 2022/23.

Pia Kipanga FC ya Zanzibar nayo imemaliza mwendo kwa kupoteza ugenini kwa kufungwa mabao 7-0 dhidi ya Club Africain hivyo nao pia safari yao imegota mwisho.

Kwenye mchezo wa kwanza walitoshana nguvu bila kufungana na mchezo wa pili Kipanga wamepoteza.

The post MPANGO WA AZAM FC, KIPANGA KIMATAIFA IMEGOMA appeared first on Saleh Jembe.

The post MPANGO WA AZAM FC, KIPANGA KIMATAIFA IMEGOMA appeared first on soka letu.

Via soka letu https://ift.tt/SxCRp9I

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT