Skip to main content

Mo Dewji aamua kukomesha, mastaa wapagawa

BAADA ya kuwaondoa Primiero de Agosto kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wachezaji wa Simba wameanza mazoezi kujiandaa na mechi ya Yanga Jumapili. Lakini kabla hawajatia mguu uwanjani akaunti zao zitakuwa zimetuna. Bilionea, Mohammed Dewji ‘Mo’ ameamua kukomesha baada ya kuhakikisha akaunti wachezaji zinanona kabla ya kufikia jioni ya leo, kutokana na ushindi bao 1-0 dhidi ya Agosto uliowapeleka kwa kishindo hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Awali juzi jioni kwenye Uwanja wa Mkapa, Kocha Juma Mgunda alitajirika baada ya kupewa minoti na wadau mbalimbali wa Simba wakiwemo wajumbe wa bodi ambao walifurahishwa na mzuka wake. Siku moja kabla ya kucheza na Agosto, viongozi wa Simba zaidi ya kumi walitembelea kambi iliyokuwa kwenye moja ya hoteli ya kifahari katikati ya Jiji la Dar es Salaam na kuwaambia wachezaji kwamba bonasi ya Mo Dewji ni Sh100 milioni lakini wao wataongeza nyingine Sh100 milioni kwa kushirikiana na wadau na wadhamini wa Simba. Miongoni mwa viongozi waliozungumza na wachezaji hao ni wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi wakiongozwa na Mwenyekiti, Salim Abdallah ‘Try Again’ pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez. Shirikisho la Soka Afrika (CAF), litaipa Simba Dola za Kimarekani 550,000 si chini ya Sh1.3 Bilioni kwa pesa za Kitanzania kama fungu ya kufuzu hatua ya makundi. Kwa mujibu wa mtandao wa CAF, umeweka kiasi cha pesa kwa timu zote 16, zilizotinga hatua ya makundi na mkwanja huo huwa unazidi kadri ambavyo timu inakwenda hatua ya mbele zaidi. PHIRI ATAMBA STRAIKA wa Simba, Moses Phiri amesema timu yake kutinga hatua ya makundi kuna maana kubwa kwao wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na mashabiki wote kwani ni miongoni mwa mafanikio kwenye msimu huu na wataongeza nguvu zaidi. “Hili la kufunga mabao matano kwenye mechi nne, nililiweka moyoni katika malengo yangu na limetimia ingawa naamini nilikuwa na nafasi ya kufunga mengine zaidi ya hayo,” alisema Phiri na kuongeza; “Mabao matano ya kwenye hatua ya awali yamepita tayari, tunakwenda kucheza mechi nyingine ngumu sita hatua ya makundi na huko nahitaji kufanya vizuri zaidi ya hatua iliyopita na hilo naamini linawezekana,” “Kufanya vizuri kwenye nafasi yangu hakuna jambo lingine zaidi ya kufunga mabao na kama nikishindwa kufanya hivyo natakiwa kuwa msahada kwa wengine kufunga mabao. “Haikuwa kazi rahisi kufunga hayo mabao bila ya ushirikiano kutoka kwa wachezaji wengine na naamini hilo tutakwenda nalo hadi katika hatua ya makundi pamoja na mashindano ya ndani.” MO AFUNGUKA “Tunafuraha kwasababu tumetinga hatua ya makundi tukiwa na kocha mzawa sio rahisi lakini imewezekana ninaimani na kocha wetu na nipo tayari kwa ushirikiano wa hali na mali ili kuweza kufikia mafanikio,” alisema na kuongeza; “Tunaelekea kwenye hatua ngumu zaidi tunaenda kukutana na wazoefu wa mashindano tunahitaji kujipanga na kutengeneza timu ya ushindani ni muhimu sana kukaa pamoja na kocha ili kuandaa mipango itakayotuvusha zaidi.” “Tulianza kwa kuchechemea tulianza tukiwa wadogo kwenye mashindano sasa ni wakubwa tunaenda kukutana na wakubwa wenzetu tunatakiwa kujipanga zaidi ili kwenda kuonyesha ubora bado naamini Simba siku moja itatwaa ubingwa wa Afrika,” alisema na kuongeza; “Nahitaji kuonana na Mgunda nina mazungumzo naye na nataka kumsikiliza ni nini anataka kwa hapa tulipofikia ili tufanyie kazi mapema kabla ya kuanza hatua nyingine ngumu,” alisema MO na kuongeza kuna dirisha la usajili mbele kama atahitaji kuongezewa nguvu wako tayari.

The post Mo Dewji aamua kukomesha, mastaa wapagawa appeared first on soka letu.

Via soka letu https://ift.tt/RXL63uz

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT