Skip to main content

Kayoko aweka rekodi

MWAMUZI Ramadhan Kayoko jana aliweka rekodi kwa mechi za dabi za hivi karibuni baada ya kugawa jumla ya kadi za njano tisa, wakati Simba na Yanga zilipopambana kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam. Katika mechi hiyo, Kayoko aligawa kadi tano za njano kwa Simba na nyingine nne kwa Yanga katika pambano hilo la 109 katika Ligi ya Bara tangu mwaka 1965. Wachezaji wa Simba waliopewa kadi hizo ni Israil Mwenda, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Mzamiru Yasin, Habib Kyombo na Augustine Okrah, wakati kwa Yanga waliolimwa ni Djuma Shaban, Stephane Aziz KI, Khalid Aucho na Feisal Salum ‘Fei Toto’. Ilikuwa ni miujiza tu kwa mwamuzi huyo kutoa kasi nyekundu kwa namna wachezaji wa timu zote walivyoonekana kukamiana na kuchezea ubabe katika dakika zote 90. Jonas Mkude angeweza kutolewa kwa kadi ya pili ya njano mapema kabla ya Fei Toto aliyekuwa na njano naye kucheza faulo ambayo ilistahili kadi ya pili ya njano. Mechi iliyokuwa inashikilia rekodi kwa kadi nyingi za dabi lilikuwa ni lile la Mei 6, 2012 wakati Yanga ikipigwa mabao 5-0 ambapo mwamuzi Hashim Abdallah alitoa njano saba na penalti tatu na kuifanya Simba ikabidhiwe taji lao kwa shangwe.

The post Kayoko aweka rekodi appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/58264/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT