Skip to main content

Huko Polisi Tanzania bado giza, warukishwa kwata Sokoine

Mbeya. Hali inazidi kuwa tete kwa Polisi Tanzania baada ya leo tena kuangukia pua kwa kisago kizito cha mabao 3-1 dhidi ya Mbeya City katika mwendelezo wa Ligi Kuu. Hiyo inakuwa mechi ya saba kwao wakicheza bila kuonja ushindi wowote wakiambulia sare mbili na kukaa mkiani kwa pointi mbili, huku Mbeya City wakichumpa hadi nafasi ya nane kwa alama tisa sawa na Tanzania Prisons, huku wakifaidika na idadi ya mabao ya kufunga. Katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Sokoine, Polisi walitumia vyema dakika 20 za kwanza kuwapelekea moto wenyeji wa mechi hiyo na kufanikiwa kupata bao la mapema dakika ya 17 kupitia kwa Vitalis Mayanga. Hata hivyo kabla ya bao hili, Maafande hao manusura wapate bao baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa City, lakini wachezaji wao walikuwa makini kuondosha hatari hiyo na kujiweka salama. Kabla ya timu hizo kwenda mapumziko, City walimpumzisha Eliud Ambokile aliyeumia na kumpisha Gasper Mwaipasi huku wakijaribu kufanya mashambulizi kadhaa lakini Kipa wa Polisi Tanzania, Christopher John alisimama imara kuokoa mikwaju yote na kufanikiwa kuipeleka timu yake kuwa salama kwa dakika 45 za kwanza wakiwa mbele. Mwamuzi wa mchezo huo, Tatu Malogo kutoka Tanga hakwenda mapumziko patupu baada ya kumuonesha kadi ya njano, Omary Chibada wa Polisi Tanzania aliyemchezea rafu kiungo wa City, Awadh Juma. Kipindi cha pili Mbeya City walirudi kwa kasi wakiwasaka wapinzani wao na dakika ya 50 waliweza kuisawazisha bao hilo kupitia kwa Hassan Nassoro aliyeunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na George Sixtus Sabilo. Dakika ya 57 Polisi Tanzania iliwatoa Fredy Tangalo na Abdul Karimu na kuwaingiza Rajabu Athuman na Jamal Mtegeta, mabadiliko ambayo hayakuonesha uhai wowote kwa timu hiyo iliyoonekana kujilinda muda wote, ikimtegemea zaidi Straika mmoja, Mayanga. Dakika ya 67 Sabilo aliiandikia bao la pili Mbeya City akiunganisha kwa kichwa mpira wa faulo ulionyooshwa na George Sangija likiwa la nne kwake msimu huu hadi sasa baada ya michezo saba kwa timu hiyo na kuwafanya Polisi Tanzania kumtoa Hassan Kapona na kuingia Idd Kipagwile. Polisi Tanzania waliendelea kuloa mabao baada ya dakika ya 69 Tariq Seif kuipatia bao la tatu Mbeya City na kuwachanganya zaidi Maafande hao ambao walionekana kuchoka zaidi. Baada ya kutupia bao hilo, Straika huyo alikimbia akitoka ndani ya uwanja akionesha ishara ya kupiga simu akimtazama Mwenyekiti wa Polisi Tanzania, aliyekuwa mwajili wake msimu uliopita, Robert Munisi aliyekuwa jukwaani na kuamsha shangwe kwa mashabiki wa City waliokuwa wakishangilia mwanzo mwisho. Dakika ya 80 timu hizo zilifanya tena mabadiliko ambapo Polisi walimtoa tena Mtegeta na kuingia Ambrose Awio, huku wenyeji wakimtoa Sangija na Awadhi Juma kuingia Ibrahim Ndunguli na Richardson Ngy’ondya.

The post Huko Polisi Tanzania bado giza, warukishwa kwata Sokoine appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/57579/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT