Skip to main content

Huko Azam mambo bado

HALI sio shwari kwa Azam FC kwani baada ya mechi tisa tu, zikiwamo saba za Ligi Kuu Bara na mbili za Kombe la Shirikisho Afrika, mabosi wa klabu hiyo wamewapiga chini makocha wawili akiwamo Denis Lavagne aliyetua mapema mwezi uliopita. Mfaransa huyo amesitishiwa mkataba wake akiitumikia timu hiyo kwa siku 45 tu tangu alipopangazwa Septemba 7, akiwa ni kocha wa pili msimu huu kwa Azam kutimuliwa, kwani alianza Abdulhimid Moallin aliyetimuliwa mapema msimu ulipoanza na kumpisha Lavagne. Akiwa Azam, Lavagne aliiongoza timu katika mechi nne za ligi, ikishinda mbili dhidi ya Mbeya City 1-0 na Singida Big Stars 1-0, huku akipoteza mbili kwa Tanzania Prisons 1-0 na KMC 2-1, katika Kombe la Shirikisho aliondoshwa na Al Akhdar ya Libya kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya kuchapwa 3-0, ugenini na kushinda 2-0, nyumbani. Mabosi wa klabu hiyo walitoa taarifa juzi ya kuachana na Lavagne na sasa timu itakuwa chini ya Kocha wa Washambuliaji, Kally Ongala akisaidiwa na nahodha Aggrey Morris anayekuwa kocha mchezaji na Mwanaspoti limepenyezewa taarifa sababu ya timua timua hiyo ya makocha ni baadhi ya viongozi wa juu kutoridhishwa na mwenendo wa timu baada ya kufanya usajili mkubwa. Chanzo hicho ambacho hakikupenda jina lake litajwe kimeeleza mabosi hawaelewi kabisa kinachoendelea kwani wametumia pesa nyingi kwenye usajili na malengo yao ilikuwa ni kufika Makundi ya Shirikisho Afrika na kumaliza ufalme wa Simba na Yanga lakini kinachotokea ni tofauti. Pia, taarifa zinaleleza huenda mabadiliko makubwa yakafanyika hivi karibuni kwenye uongozi wa timu hiyo na kuweka viongozi wapya. Lavagne amekuwa kocha wa tano kuachia ngazi kwenye Ligi Kuu msimu huu, baada ya Moallin, Zoran Maki aliyekuwa Simba, Joslin Sharif aliyekuwa Polisi Tanzania na Masoud Djuma aliyekuwa Dodoma Jiji bila kumsahau Juma Mgunda aliyehama Coastal Union na kutua Simba.

The post Huko Azam mambo bado appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/58280/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT