Skip to main content

WINGA DEMBELE ASIMULIA ALIVYOPOTEZA MIAKA MITANO

WINGA wa Klabu ya Barcelona na Timu ya Taifa ya Ufaransa Ousmane Dembele amefunguka juu ya maumivu aliyoyapitia katika miaka yake mitano ya awali akiwa na kikosi chake cha Barcelona.

Dembele ambaye kwa sasa yupo na kikosi cha Taifa cha Ufaransa kinachoshiriki michezo ya Uefa Nations amefunguka akidai kuwa miaka yake mitano ya awali akiwa na Barcelona ilipotea bure kwani alikuwa akiandamwa na majeruhi yaliyohusisha maumivu ya mara kwa mara ya misuli.

“Kuanzia mwaka 2017-2021 nilipoteza muda wangu mwingi bure, nimepoteza miaka yangu mitano, ilinilazimu nifanye kazi zaidi ili niweze kucheza, niwe na afya na ili niweze kucheza kidogo kidogo.

“Nilikuwa nikisumbuliwa na maumivu ya misuli ya mara kwa mara. Mkufunzi wangu alinisisitiza zaidi kuwa kama sitafanya mazoezi ya kutosha maumivu yangeweza kujirudia, nikiwa na Koeman nilianza kupata unafuu lakini nikiwa na Xavi hali ndiyo imeimarika zaidi. Nilivyokuja Barca nilikuwa mdogo sana, na kimsingi najiachia ndiyo lakini siyo sana kama watu wanavyosema au wanavyoweza kufikiria.” amesema Dembele.

Tangu ajiunge na klabu hiyo ya Nou Camp kwa ada ya Euro Milioni 105 kutoka Klabu ya Borussia Dortmund, Dembele amekuwa akiandamwa na majeruhi ya mara kwa mara hadi hivi karibuni alipopata fursa ya kuepukana na majeraha na kuwa katika kiwango kikubwa akiisaidia klabu yake na sasa ameitwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Ufaransa.

The post WINGA DEMBELE ASIMULIA ALIVYOPOTEZA MIAKA MITANO appeared first on Saleh Jembe.

The post WINGA DEMBELE ASIMULIA ALIVYOPOTEZA MIAKA MITANO appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/55699/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT