Skip to main content

Wapiganaji wa Tigray wakubali kushiriki mchakato wa amani unaosimamiwa na AU

Tangazo hilo lilitolewa huku kukiwa na juhudi mbalimbali za diplomasia ya kimataifa baada ya mapigano kupamba moto mwezi uliopita kwa mara ya kwanza katika miezi kadhaa kaskazini mwa Ethiopia.

“Serikali ya Tigray iko tayari kushiriki katika mchakato thabiti wa amani chini ya mwamvuli wa Umoja wa Afrika,” ilisema taarifa ya mamlaka ya Tigray.

“Zaidi ya hayo, tuko tayari kutii usitishaji wa mara moja na uliokubaliwa kwa pande zote mbili wa uhasama ili kuweka mazingira mazuri,” iliongeza.

Serikali ya Ethiopia hapo awali ilisema iko tayari kwa mazungumzo yasiyo na masharti “wakati wowote, mahali popote,” yaliyosimamiwa na AU yenye makao yake makuu mjini Addis Ababa.

Chama cha Tigray People’s Liberation Front (TPLF) hadi sasa kilikuwa kimepinga vikali jukumu la mjumbe wa AU katika Pembe ya Afrika Olusegun Obasanjo, kikilalamikia “ukaribu” wake na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed.

Mkuu wa Tume ya AU Moussa Faki Mahamat alitoa taarifa ya kukaribisha hatua hiyo kama “fursa ya kipekee kuelekea kurejesha amani” na kuzitaka “pande zote mbili kufanya kazi kwa haraka kuelekea usitishaji mapigano mara moja, na kushiriki katika mazungumzo ya moja kwa moja”.

The post Wapiganaji wa Tigray wakubali kushiriki mchakato wa amani unaosimamiwa na AU appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/54029/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT