Skip to main content

UBABE UBABE TU MTWARA, KIDUKU, MANDONGA MTU KAZI KAZINI

MASAA machache yamesalia kutoka hivi sasa leo Jumamosi Septemba 24, 2022 mabondia Twaha Kiduku na Abdo Khaled raia wa Misri kupanda ulingoni kuwania mkanda wa UBO Intercontinental kutoka Mtwara Ubabe Ubabe linalotarajia kupigwa kwenye Uwanja wa Nangwanda wa Sijaona mkoani Mtwara.

Kiduku na Khaled wa wamepima uzito na tayari kwa pambano hilo la uzani wa Super Middle ambalo litachezwa kwa raundi 10 huku wa kazi wa mkoani hapa wakitarajia kushuhudia  kutoka kw mabondia hao.

Licha ya kuwepo kwa mapambano ya utangulizi ila bondia Karim Mandonga  amekuwa gumzo kubwa kwa watu wa mjini hapa kutokana na  umaarufu wa bondia huyo kutoka Morogoro kufuatia mikwara anayowapiga mabondia wenzake licha  ya kupokea vichapo mara kwa mara.

Kiduku amewahakikishia Watanzania kuwa yupo tayari kuwapa burudani ya ushindi kwenye pambano hilo wakati mpinzani wake akisema  kuwa atamaliza raundi kumi za pambano hilo kwa kuamini atamchapa mpinzani wake.

Mbali ya Kiduku, bondia Karim Mandonga ‘Mtu Kazi’ aliyepewa ubalozi wa mkoa wa  hapa, ameendelea kuonyesha umaarufu wake kuliko wanasumbwi wengine waliombatana.

Mandoga  atacheza na Salim Abeid pambano la raundi nne, Adam Lazaro atatwangana na Francis Miyeyusho, Emiliano Polino atacheza na Osama Arabi.

Selemani Galile atapambana na Shaban Ndaro pambano la raundi sita, uzito wa kati, Nasra Msami dhidi ya Halima Bandola ikiwa ndiyo pambano pekee la wanawake likiwa la raundi sita

Alto Kyenga atapambana na Ibrahim Tamba raundi sita, Malik Deo atacheza dhidi ya Bosco Bakari pambano la raundi nne, Paschal Manyota atazichapa dhidi ya Joseph Mchapeni.

Mapambano mengine ni Shafii Mohamed dhidi ya Ramadhan Sunya, Iddi Pazi atacheza na Sebaatian Temba, Ayoub Mwankina dhidi ya Shaban Rajabu, Yassin Mbegu dhidi ya Hassan Mgaya. Azizi Salumu dhidi ya Biemo Max.

The post UBABE UBABE TU MTWARA, KIDUKU, MANDONGA MTU KAZI KAZINI appeared first on Saleh Jembe.

The post UBABE UBABE TU MTWARA, KIDUKU, MANDONGA MTU KAZI KAZINI appeared first on soka letu.

Via soka letu https://ift.tt/GMIegZV

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT