Skip to main content

Simba Yavamia Angola, Yapiga Mkwara Mzito Clube Desportivo 1º de Agosto



Simba Yavamia Angola, Yapiga Mkwara Mzito Clube Desportivo 1º de Agosto

Wachezaji wa Simba.

UONGOZI wa Simba umewaambia wapinzani wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Clube Desportivo 1º de Agosto ya nchini Angola kuwa kamwe hawatakubali kufanyiwa vitendo vya kihuni kuanzia ndani hadi nje ya uwanja na wao wakakaa kimya, ni lazima watajibu mapigo.

Kauli hiyo imetolewa wakati Simba ikijiandaa kwenda kuvaana na Clube Desportivo 1º de Agosto katika hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika mchezo ambao utapigwa kati ya Oktoba 7-9, mwaka huu huko nchini Angola.

Simba itavaana dhidi ya Agosto baada ya kufanikiwa kuwaondoa Nyasa Big Bullets kwa ushindi wa jumla mabao 4-0.

Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema kuwa uongozi unafahamu uhuni wote wanaoufanya Clube Desportivo 1º de Agosto wakiwa nyumbani kwao, hivyo wamejiandaa kupambana nao.

Ally alisema kuwa kamwe hawatavumilia vitendo vya kihuni watakavyovifanya wapinzani wao wakiwa nyumbani kwao, badala yake watalipiza huko ugenini kabla ya kurudiana hapa nyumbani.

Clube Desportivo 1º de Agosto

Aliongeza kuwa, uongozi umejipanga katika kila kitu kitakachotokea ugenini baada ya kuanza maandalizi ya kuhakikisha wanapambana na kila hujuma itakayotokea.

“Tumepanga kuwahi mapema Angola kwa maana ya viongozi kuandaa mazingira mazuri itakayofikia timu kwa maana ya hoteli, uwanja wa kufanyia mazoezi pamoja na chakula.

“Hiyo ni baada ya kuujua uhuni wote kwa maana ya hujuma wanazotumia, kama uongozi tumejiandaa na kila uhuni watakaoufanya wa ndani na nje ya uwanja.

“Hivyo wakae wakijua kwamba hatutavumilia kwa kila uhuni watakaoufanya mara baada ya kuingia katika ardhi ya Angola, tena wasijaribu kabisa kingine wafahamu kabisa lazima na wao waje hapa nchini,” alisema Ally.

STORI: WILBERT MOLANDI







Toa comment

The post Simba Yavamia Angola, Yapiga Mkwara Mzito Clube Desportivo 1º de Agosto appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/55529/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT