Skip to main content

Ruto kuapishwa leo

Hafla ya uapisho itafanyika katika uwanja wa kimataifa wa michezo wa Kasarani, nje kidogo ya mji mkuu, Nairobi.

Kwa mujibu wa katiba ya Kenya, rais mtele ni lazima aapishwe kati ya Saa nne asubuhi na saa nane mchana.

Mahakama ya juu ya Kenya iliamuru Jumatatu wiki jana kwamba Ruto alimshinda mpinzani wake wa karibu, Raila Odinga, katika uchaguzi wa urais uliofanyika tarehe tisa mwezi Agosti, baada ya Odinga kupinga matokeo yaliyokuwa yametangazwa na tume ya uchaguzi na mipaka, IEBC.

Jumatatu, Ruto alikutana na rais anayeondoka Uhuru Kenyatta kwenye ikulu mjini nairobi, huku mchakato wa kukabidhiana mamlaka, ulioanza Jumanne wiki jana ukiendelea.

“Tumekamilisha matayarisho ya hafla hiyo na ni matumaini yetu kwamba itafanyika kwa amani,” alisema kaimu mwenyekiti wa tume ya ukabidhianaji madaraka, Karanja Kibicho, akizungumza na waandishi wa habari Jumatatu mjini Nairobi.

Rais Uhuru Kenyatta, ambaye awali hakuwa amempongeza naibu wake William Ruto moja kwa moja kwa ushindi wake, alitoa pongezi katika hotuba yake na kumtakia kila la heri kama kiongozi ajaye wa nchi hiyo.

Darzeni za viongozi wa nchi na serikali wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo.

Tunatarajia takriban watu 60,000 kuhudhuria hafla hiyo, wakiwemo viongozi wa nchi na serikali waptao 20 kutoka sehemu mbalimbali. Tuko tayari kabisa,” alisema Kibicho.

Wakati huo huo, Odinga ambaye hajazungumza moja kwa moja na Ruto tangu mahakama kutoa uamuzi wake, amesema hatahudhuria hafla hiyo ya uapisho.

Odinga alisema yuko nje ya nchi, na kwamba ana mashaka mengine. Katika taarifa, mwanasiasa huyo mkongwe alikiri kwamba alikuwa amepokea mwaliko.

Alichukua fursa hiyo kuinyooshea kidole Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kwa “kutotenda haki katika kuendesha uchaguzi huo.”

Alisema ingawa yeye na muungano wa kisiasa aliouwakilisha waliheshimu uamuzi wa mahakama ya juu, hawakukubaliana na jinsi ilivyoshughulikia kesi hiyo.

The post Ruto kuapishwa leo appeared first on soka letu.

Via soka letu https://ift.tt/3PmlAEV

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT