Skip to main content

Akpan nje wiki tatu

KIUNGO mkabaji wa Simba, Victor Akpan atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu na kumfanya akose maufundi ya kocha aliyemnoa akiwa Coastal Union, Juma Mgunda aliyejiunga na Wekundu hao wa Msimbazi kwa sasa.
Akpan alijiunga na Simba mapema msimu huu akitokea Coastal iliyokuwa chini ya Mgunda akiwa ndiye chaguo lake la kwanza kutokana na kumchezesha kikosi cha kwanza kwa msimu mzima ikiwamo kupiga shoo ya maana kwenye fainali ya ASFC dhidi ya Yanga iliyopigwa jijini Arusha, Julai 2.
Akizungumza na Mwanaspoti, Akpan alisema kuwa kwake nje ya timu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mguu aliyoyapata katika michezo ya kirafiki iliyochezwa nchini Sudan kutamnyima fursa ya kuanza kazi upya na Mgunda ndani ya Simba. “Nilicheza mechi moja tu dhidi ya Asante Kotoko kati ya michezo miwili ambayo Simba ilicheza Sudan ukiwamo wa wenyeji wa michuano hiyo maalum, Al Hilal na kuumia na jeraha hilo litaniweka nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu, japo naendelea na mazoezi mepesi gym,” alisema Akpan na kuongeza; “Najisikia vibaya kwa vile ninahitaji kucheza zaidi kutokana na kuingia kwenye timu hivi karibuni lakini ni mipoango ya Mungu nikiwa fiti nitarudi uwanjani kuendelea na majukumu yangu kama kawaida na nitafurahi kukutana tena na kocha Mgunda aliyeniamini tulupokuwa Coastal.”
Akpan alisema anatamani angemkuta akiwa fiti ili aweze kumtumia kama alivyokuwa naye hapo awali lakini anaamini muda bado upo atakutana naye na kufanya kile anachokiamini kuwa anacho mguuni mwake. “Nimepokea kwa furaha ujio wa Mgunda ndani ya Simba bahati mbaya amekuja kipindi ambacho nipo nje ya timu nikiuguza majeraha lakini naamini kwa muda ambao ntakuwa nje atakuwa bado anainoa Simba nitakutana naye,” alisema na kuongeza; “Ni kocha mzuri anauwezo mkubwa naamini ataisaidia Simba kufikia mafanikio kama amepewa muda mrefu wa kuinoa timu hiyo huku akisisitiza kuwa ni kocha ambaye anaamini katika vipaji na uwezo wa mchezaji.”

The post Akpan nje wiki tatu appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/55385/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT