Skip to main content

Wizara zahimizwa kufuatilia taarifa za mpango kazi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Viongozi wa Wizara nchini zimepewa rai kufuatilia na kusimamia kwa karibu maafisa viungo ambao wanahusika kuweka taarifa kwenye mfumo ili Viongozi wawe na umiliki (ownership) wa taarifa zilizo katika mfumo huo.

Hayo yamesemwa leo Agosti 11, 2022 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene katika kikao kazi cha Mawaziri kilichofanyika katika Ukumbi wa Kambarage Hazina jijini Dodoma.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Stergomena Tax akizungumza jambo na Naibu Waziri Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani Kikwete kabla ya kuanza kwa kikao kazi cha Mawaziri kilichofanyika Ukumbi wa Kambarage jijini Dodoma.

“Kwa upande wa uwasilishaji wa Taarifa ya Ilani ya Chama Tawala, uchambuzi umeonesha kuwa kwa kipindi cha mwaka 2022 ni Wizara 14 pekee zilizowasilisha Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Ilani kwa mwaka 2022 na Wizara 13 hazijawasilisha.

“Taarifa za Mpango kazi hutakiwa kuwasilishwa kwenye Mfumo wa ‘DASHBOARD’ mwezi Januari kila mwaka. Aidha, kwa upande wa Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani kwa kipindi cha nusu mwaka, ambazo hutakiwa kuwasilishwa Julai 2022 ni wizara 4 zilizowasilisha,” amesema Simbachawene.

Amesema kwa mwaka 2022 wamepokea maelekezo yako kuwa Taarifa ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuhusu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 na Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kuhusu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 itawasilishwa mwezi Novemba, 2022.

“Ili kuratibu taarifa hiyo vyema na kwa wakati, napenda Mawaziri kuratibu taarifa katika maeneo yanayowahusu na kuhakikisha zinawasilishwa kwa wakati kupitia mfumo huo,” amesema Simbachawene.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu, Dk. John Jingu akiwa katika Kikao kazi cha Mawaziri kilichofanyika Ukumbi wa Kambarage hazina Jijini Dodoma.

The post Wizara zahimizwa kufuatilia taarifa za mpango kazi appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/45918/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT