Waziri Mkuchika : Msiwafiche wenye ulemavu kuhesabiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Maalum George Mkuchika amewataka wazaz…

Waziri Mkuchika : Msiwafiche wenye ulemavu kuhesabiwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Maalum George Mkuchika amewataka wazazi na walezi nchini kutowaficha watoto wenye ulemavu wakati wa zoezi la sensa ya watu na makazi.
Waziri Mkuchika amesema watu wenye ulemavu wana haki ya kuhesabiwa kama watu wengine, hivyo ni vema wahesabiwe kwa kuwa takwimu zao ni muhimu kwa mipango ya maendeleo.
Amesema wapo viongozi mbalimbali ndani ya serikali ambao wana ulemavu, ambapo kama wazazi ama walezi wao wangewaficha wasingeweza kupata elimu.
Waziri Mkuchika amesema wakati umefika kwa serikali kufahamu idadi ya watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali ili kuona namna ya kuwasaidia.
Kwa mujibu wa Waziri Mkuchika, kupatikana kwa takwimu sahihi za watu wenye ulemavu kutaisaidia serikali kuandaa miundimbinu yao katika maeneo muhimu kama vile kwenye sekta ya elimu.

The post Waziri Mkuchika : Msiwafiche wenye ulemavu kuhesabiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Maalum George Mkuchika amewataka wazaz… appeared first on soka letu.
source https://mjombazecoder.website/48694/
Comments
Post a Comment