Skip to main content

Mikhiel Gorbachev, rais wa mwisho wa Urusi, aaga dunia akiwa na umri wa miaka 91

Gorbachev, kiongozi wa mwisho wa Urusi, alishiriki pakubwa katika mikataba kati ya Muungano wa Usovieti na Marekani ya kutaka kupunguza silaha, na ushirikiano na madola ya Magharibi ili kuondoa wingu nzito la mgawanyiko wa Ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia na kupelekea muungano wa Ujerumani.

Lakini mageuzi yake mapana ya ndani yalisaidia kudhoofisha Umoja wa Kisovieti hadi ikasambaratika, muda ambao Rais Vladimir Putin ameuita “janga kubwa zaidi la kisiasa la kijiografia” la karne ya ishirini.

“Mikhail Gorbachev amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua ugonjwa mbaya na wa muda mrefu,” Hospitali Kuu ya Russia ilisema katika taarifa.

Putin alitoa “rambi rambi zake,” msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov aliambia shirika la habari la Interfax.

“Kesho atatuma ujumbe wa rambirambi kwa familia na marafiki,” alisema. Mnamo mwaka wa 2018, Putin alisema angebadilisha kuanguka kwa Umoja wa Kisovieti ikiwa angeweza, mashirika ya habari yaliripoti wakati huo.

Viongozi wa dunia walikuwa wameendelea kutuma risal za rambirambi kufuatia kifo cha Gorbachev.

Mkuu wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen alisema Gorbachev amefungua njia kwa Ulaya huru.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, akitoa mfano wa uvamizi wa Putin nchini Ukraine, akisema “kujitolea bila kuchoka kwa Gorbachev kufungua jumuiya ya Sovieti bado ni mfano kwetu sote”.

The post Mikhiel Gorbachev, rais wa mwisho wa Urusi, aaga dunia akiwa na umri wa miaka 91 appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/51691/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT