Skip to main content

Waziri Makamba atatua changamoto ya umeme Sengerema

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Nishati, January Makamba ametatua changamoto ya muda mrefu ya kutopata umeme wa uhakika  wilayani Sengerema kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukatika kwa laini iliyokuwa ikipeleka umeme wilayani humo kutokea Mwanza ambako kulisababishwa na shughuli za ujenzi wa Daraja la Busisi na kupelekea umeme kukatika zaidi ya mara 10 kwa siku.

Waziri wa Nishati, January Makamba akizindua huduma ya umeme katika Shule ya Msingi ya Kizugwangoma inayofundisha watoto wenye mahitaji maalum.

Waziri wa Nishati alitatua changamoto hiyo Julai 14, 2022 baada ya kufika wilayani humo ikiwa ni sehemu ya ziara yake siku 21 katika mikoa 14 nchini ambapo pamoja na kukagua miradi inayotekelezwa na Wizara ya Nishati kupitia Taasisi zake, ziara hiyo imelenga kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.

“Sababu za kutokuwa na umeme wa uhakika wilayani hapa ni uchakavu wa miundombinu na kukua kwa mahitaji, lakini sisi pia hatukufanya kazi ya kupanua na kuboresha miundombinu ili kuendana na mahitaji ya sasa. Awali, Sengerema ilikuwa ikipata umeme kutoka njia ya Geita na Mwanza lakini njia ya mwanza ilikatika kwa bahati mbaya, hivyo kufanya Sengerema kupata umeme kutokea Geita pekee ambao hautoshi.” Alisema Makamba

Ili kutatua changamoto hiyo, Waziri Makamba alisema kuwa, hadi kufikia mwezi wa 10 mwaka huu itajengwa njia nyingine ya umeme kutokea kituo cha Mpomvu Geita ambayo itapeleka umeme wa megawati 20 wilayani humo na hivyo kukidhi mahitaji kwani kwa sasa matumizi ya umeme ya Sengerema ni megawati 5 hadi 6.

Aliongeza kuwa, Daraja la Busisi litakapomalizika itajengwa tena laini ya umeme kutokea jijini Mwanza na hivyo kufanya Wilaya hiyo kuwa na uhakika zaidi wa upatikanaji umeme na kwamba kutakuwa na laini nyingine ya kV 220 ambayo itapita pia wilayani humo ambayo imelenga kupeleka umeme kwenye migodi.

Waziri wa Nishati, January Makamba akizungumza na Kikundi cha  Mamalishe Busisi ikiwa ni sehemu ya umasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia ambapo aliwapatia pia mitungi ya gesi ili kurahisisha shughuli zao za upishi na pia kuepukana na athari za kuni na mkaa.

Kuhusu umeme vijijini, alisema kuwa Wilaya hiyo ina vijiji 153 na tayari vijiji 143 vimeshasambaziwa umeme na kwamba Vijiji 10 vilivyobaki vinaendelea kusambaziwa umeme kupitia mradi wa umeme vijijini wa Awamu ya Tatu, mzunguko wa Pili.

Akiwa wilayani Sengerema, Waziri wa Nishati  aligawa mitungi ya gesi takriban 80 ili kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ambapo alifafanua kuwa, hiyo ni programu maalumu ya majaribio ambayo itawezesha upatikanaji wa taarifa zitakazozewesha kutengeneza mpango mkubwa wa kitaifa wa usambazaji wa gesi nchini na kwamba programu hiyo ni ya miezi Sita na wanufaika ni kinamama.

Kuhusu usambazaji umeme visiwani, alisema kuwa Sh bilioni 54 zimetengwa kwa ajili ya kusambaza umeme kwenye visiwa takriban 47 nchini huku visiwa 35 vikiwa ndani ya Ziwa Victoria.

Waziri wa Nishati, January Makamba akizungumza na Wananchi wilayani Sengerema ambapo aliwaeleza kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali ili kutatua changamoto ya upatikanaji wa umeme wa uhakika wilayani humo.

Waziri wa Nishati, pia aliwasha umeme katika shule ya watoto wenye mahitaji maalum ya Kizugwangoma ambapo Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Benedicto Bijiga alimweleza Waziri kuwa, umeme huo sasa unawawezesha wanafunzi hao wenye mahitaji maalum kujifunza kwa kutumia luninga, kupata burudani na pia kurahisisha matumizi mengine kama ya kuchapa na kudurufu mitihani. 

The post Waziri Makamba atatua changamoto ya umeme Sengerema appeared first on soka letu.

Via soka letu https://ift.tt/bS2mlDO

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT