Skip to main content

Wataalamu wanaosimamia miradi watakiwa kufuata kanuni na taratibu ili kupata miradi yenye ubora

Na Clara Matimo, Buchosa

Wataalamu waliopewa dhamana na Serikali ya kuisimamia miradi wametakiwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa ikiwemo  kushiriki kikamilifu katika vikao vyote vya ujenzi ili kuhakikisha inatekelezwa kwa ubora

Agizo hilo limetolewa  Julai 18, 2022 na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, 2022, Sahili Geraruma, wakati akizindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Buchosa Mkoani Mwanza ikiwemo ya maji, elimu na afya iliyogharimu Sh milioni 735,754,300.

Amesema mwenge wa uhuru umebaini kwamba wataalamu wengi pamoja na watendaji katika halmashauri nyingi nchini wanashiriki kikamilifu kwenye miradi inayopitiwa na mwenge huo lakini ambayo haipitiwi huwaachia  madiwani, walimu na watendaji wa kata wakati hawana utaalamu wa masuala ya ujenzi.

Amesema ameridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo  lakini kasoro ndogo alizozibaini ambazo zinarekebishika zisingekuwepo endapo wataalamu wangeshiriki kikamilifu katika ujenzi  na kutoa ushauri.

“Niwapongeza kwa usimamizi mzuri wa miradi hii ambayo mwenge wa uhuru umeipitia naomba jitihada ambazo wataalamu wameweka katika miradi yote iliyopitiwa na mwenge waziweke pia kwenye miradi mingine ambayo haipitiwi na mwenge ili iwe na ubora iweze kuwanufaisha wananchi kwa muda mrefu, Tanzania ni  yetu inabidi ipendeze,”amesisitiza Geraruma.

Akitoa taarifa ya mradi wa maji uliojengwa katika kijiji cha Magulukenda kabla haujazinduliwa na Geraruma, Kaimu Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Sengerema, Mhandisi Venslaus Blaise amesema hadi umekalimika umegharimu Sh milioni 150 kutoka Serikali kuu.

“Mradi huu ulianza kutekelezwa Mei, 2020 lengo ni kutoa huduma ya maji safi kwa wakazi 5151 katika maeneo ya kijiji hiki cha Magulukenda, kukamilika kwa mradi huu kumeleta manufaa mengi kwa jamii ikiwemo kuimarisha uchumi kwa wananchi kwa kuondo muda wa kutafuta maji.

“Faida zingine ni kuchochea ukuaji wa miji hasa baada ya kuwepo huduma ya maji, kuwepo kwa shughuli za kimaendeleo mfano umwagiliaji wa mashamba, kuchochea na kuimarisha hali ya usalama katika kijiji,”ameeleza Mhandisi Blaise.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Erick Shigongo, ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kupeleka fedha katika jimbo hilo kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwemo ya Afya,maji na miundombinu ya barabara.

“Nimesimama hapa kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Buchosa kukuomba kiongozi utupelekee shukurani zetu wana Buchosa kwa Mheshimiwa Rais Samia kwa fedha alizotuletea na anazoendelea kutuletea wananchi wa Buchosa kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo,” amesema Shigongo.

Awali, akipokea Mwenge wa Uhuru eneo la Iseni Halmashauri ya Buchosa Mkuu wa Wilaya  ya Sengerema, Senyi Ngaga, amebainisha kwamba mwenge wa Uhuru utakimbizwa jumla ya kilomita 94.7 ambapo utapitia miradi mitano yenye thamani ya Sh 735,754,300, kati ya hiyo mitatu itazinduliwa, mmoja utawekewa jiwe la msingi na mmoja ni  kukabidhi vifaa kwa kikundi cha vijana.

The post Wataalamu wanaosimamia miradi watakiwa kufuata kanuni na taratibu ili kupata miradi yenye ubora appeared first on soka letu.

Via soka letu https://ift.tt/GgTh7pa

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT