Skip to main content

Wakuu wa idara, wataalamu watakiwa kumaliza hoja za CAG

Na Clara Matimo, Mwanza

Wakuu wa Idara na Wataalamu kutoka sekta mbalimbali Mkoani Mwanza wametakiwa kwenda katika halmashauri zote nane zilizopo mkoani humo ili kushirikiana na wenzao wa maeneo hayo kujibu hoja za Mdhibiti  na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali  (CAG) kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

Agizo hilo limetolewa mkoani hapa Julai Mosi na Mkuu wa Mkoa huo, Mhandisi Robert Gabriel, wakati akizungumza na watumishi wa Ofisi yake kwenye kikao kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya kiutumishi na maendeleo kwa mwaka wa fedha ulioishia juni 30, 2022.

Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakiwa kwenye kikao kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya kiutumishi na maendeleo kwa mwaka wa fedha ulioisha juni 30, 2022.Kikao hicho kiliwakutanisha na Mkuu wa Mkoa huo, Mhandisi Robert Gabriel pamoja na Katibu Tawala, Ngusa Samike

Alieleza kwamba hivi karibuni amezunguka katika halmashauri zote za mkoa huo kwenye mkutano maalumu wa baraza la madiwani uliolenga kujadili utekelezaji wa hoja za CAG kwa mwaka wa fedha 2020/2021 amebaini changamoto kadhaa hivyo ni wajibu wa watumishi hao ngazi ya mkoa kuwasaidia ili kuziondoa na kuepuka matumizi mabaya ya fedha .

“Hoja za CAG  zipewe kipaumbele kwa mwaka mpya wa fedha ulioanza Julai Mosi, mwaka huu kwani mafanikio ya mtu mmoja ni Yetu sote na  kushindwa kwa kitengo kimoja ni kushindwa kwetu wote tuangalie ndoto dira na mwelekeo wa serikali.

“Tuweke malengo kwenye mwaka huu mpya wa fedha tunataka tufike wapi, malengo yanaokoa muda usipokuwa na malengo utabaki kuzunguka tu maana haujui unapokwenda, nawaombea kila mtumishi Mwenyezi Mungu awaongezee ufanisi wa ziada katika kutimiza majukumu yenu, vitengo vyote tuwe sehemu ya suluhu na ufanisi wa utendaji kazi,” alisema na kuongeza.

 “Mimi ninyi siwaoni kama ni wafanyakazi wenzangu nawaona kama ni ndugu zangu wa damu, kikao hiki mbali na kufanya tathmini kinatusaidia kujuana mkijuana mnaaminiana tujifunze kuombeana, kuvumiliana na kusameheana ili tufanye kazi zenye tija,”alisema.

  Aidha amewataka kufanya tathmini ya kina ya vyanzo vya mapato ndani ya mkoa, ili kubaini vinavyohitaji maboresho maana mapato yakiongezeka wanajenga msingi mzuri katika kutatua changamoto mbalimbali ndani ya mkoa na taifa kwa jumla.

“Tunapofungua  mwaka mpya wa fedha 2022/23 tumekutana ili kufanya tathmini ya kazi tulizotekelezwa katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita hongereni kwa kazi nzuri mliyofanya mwaka huu mpya tuna deni kubwa katika kuwahudumia wananchi kupitia ofisi zetu hivyo pamoja na tathmini tunayoenda kufanya ni wajibu wetu kuongeza ushirikiano na kuombeana kheri katika kazi,”alisema.

Ametaja mafanikio ya kiutumishi kwa mwaka wa fedha  2021/2022 kuwa ni pamoja na watumishi 51 wa kada mbalimbali wamepandishwa vyeo kuanzia Juni 2021 hadi Mei 2022 na wengine idadi hiyo hiyo wamethibitishwa vyeo, kiasi cha Sh milioni 436,749,786 kimelipwa kwa wazabuni waliokuwa na madai mbalimbali ya miaka ya nyuma.

“Kiasi cha Sh milioni 209, 167,830 kimelipwa kwa watumishi waliokuwa wakidai madai yasiyo ya mishahara, tumefanikisha kuandaa bajeti ya mishahara ya watumishi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo kiasi cha Sh milioni 185,844,000 kimetengwa kwa ajili ya ajira mpya kati ya hizo 14 kada za udereva, RMAs, PSs pamoja na kupandishwa vyeo watumishi 29,”alisema Mhandisi Gabriel.

Naye, Katibu Tawala wa Mkoa huo  Ngusa Samike, amemshukuru  Rais Samia Suluhu Hassan,  kwa kuipatia Ofisi hiyo Sh  Bilioni 1.75 ambazo zinatekeleza maboresho ya miundombinu pamoja na ujenzi wa nyumba za Makatibu Tawala Wasaidizi, Ukarabati wa Ofisi za Wakuu wa Wilaya na Ujenzi wa Ofisi za Maafisa Tarafa.

CAPTION

KATIBU TAWALA : , Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Ngusa Samike, akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye kikao kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya kiutumishi na maendeleo kwa mwaka wa fedha ulioisha juni 30, 2022.

WATUMISHI :

The post Wakuu wa idara, wataalamu watakiwa kumaliza hoja za CAG appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/31656/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT