Skip to main content

REA yaeleza ilivyoboresha maisha ya wananchi vijijini

Na Veronica Simba, REA

MIRADI ya umeme vijijini inayoendelea kutekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imechangia kuboresha maisha ya wananchi wa maeneo hayo.

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam leo Julai 3, 2022 na Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka REA, Mhandisi Jones Olotu alipokuwa akizungumza na waandshi wa habari. 

Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhandisi Francis Songela (kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka REA, Mhandisi Jones Olotu (kulia), wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mjasiriamali anayeuza majiko yanayotumia nishati kidogo, wakati wa Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa, Julai 3, 2022 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika Banda la REA lililopo kwenye Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa (SabaSaba), Mhandisi Olotu amesema, umeme vijijini umewapatia wananchi fursa ya kufanya kazi mbalimbali za ujasiriamali hivyo kujiongezea kipato.

Amezitaja baadhi ya kazi hizo kuwa ni pamoja na kuchomelea vyuma, saluni za kike na kiume pamoja na mashine za kusaga nafaka.

Aidha, ameongeza kuwa upatikanaji wa umeme vijijini umewezesha kuboresha huduma mbalimbali zitolewazo kwa umma ikiwemo afya na elimu. 

Kwa upande wake, Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhandisi Francis Songela, amesema kwamba REA imejipanga kuhakikisha inafikisha nishati hiyo katika maeneo yote vijijini, awamu kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. 

Akifafanua, Mhandisi Songela amesema REA inatambua kiu kubwa ya umeme waliyonayo wananchi vijijini, ndiyo maana kazi ya kupeleka nishati hiyo ni endelevu ikilenga kuvifikia vijiji na vitongoji vyote.

Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini, Mhandisi Francis Songela akisaini Kitabu cha Wageni, alipotembelea Banda la REA katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa, Julai 3, 2022 jijini Dar es Salaam.

The post REA yaeleza ilivyoboresha maisha ya wananchi vijijini appeared first on soka letu.

Via soka letu https://ift.tt/DmuoJc5

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT