Skip to main content

Mkenya Cherono na Marekani Ross wasitishwa mashindano mabingwa wa riadha duniani

AIU, inayosimamia masuala ya uadilifu katika riadha ya kimataifa ikiwa ni pamoja na utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu, imesema vipimo vilivyofanyiwa Cherono vimegundua kwamba ametumia dawa ya aina ya trimetazidine.

Hiyo ni moja kati ya dawa zilizoko kwenye orodha ya Idara ya kupambana na dawa za kuongeza nguvu zilizopigwa marufuku kwa mwaka 2022.

Cherono mshindi wa mbio za marathon za Boston na Chicago mwaka 2019, alitoa sampuli ya damu na mkojo wake kabla ya mashindano hapo May 23 na kuarifiwa matokeo alipofika Eugene siku ya Alhamisi.

Kwa upande wa Ross, taarifa ya AIU ina sema mwanariadha huyo aliyeshiriki katika timu ya mbiyo za mita 400 kupokezana iliyoshinda nishani ya dhahabu mwaka jana kwenye mashindano ya Olympiki amesitishwa kutokana na tabia yake wakati wa uchunguzi kuweza kufahamu mahala alikuwepo.

Mashindano yote ya awali ya Marathon na mita 400 yanafanyika Jumapili kwa hivyo hawatoweza kushiriki.

The post Mkenya Cherono na Marekani Ross wasitishwa mashindano mabingwa wa riadha duniani appeared first on soka letu.

Via soka letu https://ift.tt/lXB9LOg

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT