Skip to main content

YANGA KUIKABILI MBEYA CITY


KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi leo kitakuwa na kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Mbeya City kwenye mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Jana wachezaji wa Yanga ikiwa ni pamoja na Zawad Mauya, Fiston Mayele,Feisal Salum walikuwa ni miongoni mwa nyota ambao walifanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya kueleka mchezo wa leo.

Pia wanatarajiwa kuweza kukabidhiwa taji lao la Ligi Kuu Bara ambalo ni la 28 kwao baada ya kuweza kuwavua ubingwa msimu huu mabingwa watetezi Simba.

Cedrick Kaze, Kocha Msaidizi wa Yanga ameweka wazi kwamba wanatambua mchezo utakuwa mgumu lakini wapo tayari kwa ajili ya kupata pointi tatu muhimu.

“Mchezo tunatambua kwamba utakuwa mgumu lakini tupo tayari kwa ajili ya ushindani na tunaamini kwamba tutapata pointi tatu kwa kuwa sherehe za ubingwa zimekwisha.

“Ambacho tunakifanya ni kuendelea kulinda rekodi yetu tusipoteza mchezo kwani wachezaji wanajua kwamba kila timu tunayokutana nayo inahitaji kutufunga,” amesema.

Kwenye msimamo Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 70 aada ya kucheza mechi 28 inakutana na Mbeya City iliyo nafasi ya 9 na pointi 35.

Yanga imetoka kuwashushia kichapo cha mabao 2-0 Polisi Tanzania kwenye mchezo wao uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

The post YANGA KUIKABILI MBEYA CITY appeared first on Saleh Jembe.

The post YANGA KUIKABILI MBEYA CITY appeared first on soka letu.

Via soka letu https://ift.tt/z2IZnL9

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT