Skip to main content

Waziri Ndalichako: Serikali inatambua mchango wa sekta binafasi katika kukuza uchumi

Na: Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan inathamini na kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Sekta Binafsi katika ukuaji wa ajira na uchumi nchini.

Ameyasema hayo wakati wa Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 63 wa mwaka wa Chama cha Waajiri uliofanyika Jijini Dodoma Juni 22, 2022. Amefafanua kuwa Sekta Binafsi ni msingi wa ukuaji wa ajira, na ni injini ya uchumi wa nchi yetu.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi akieleza jambo wakati wa Mkutano huo.

Prof. Ndalichako, amefafanua kuwa sekta binafsi inatoa mchango mkubwa katika uzalishaji wa bidhaa na uwekezaji katika sekta za kimkamakati. Aidha, amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Waajiri wote hususani wa Sekta Binafsi katika kuibua fursa za maendeleo, kujadili changamoto zao na kuzipatia ufumbuzi kwa haraka.

“Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ina imani kubwa na ATE na Waajiri wote katika kuleta mageuzi ya kiuchumi nchini,” amesema Prof. Ndalichako.

Ameongeza kuwa Ofisi hiyo imeendelea kushirikiana na Wadau wa Utatu (Serikali, Wafanyakazi na Waajiri) hususani katika kuboresha mahusiano mahali pa kazi na kulinda Sekta Binafsi kama mdau muhimu wa uchumi nchini.

Ameeleza masuala ambayo serikali inaendelea kushirikiana na wadau wa utatu ni pamoja na mapitio ya Kanuni za Mafao kwa Wastaafu kwa watumishi wote wa Sekta ya Umma na Binafsi. Pia, inaendelea kupanga kima cha chini cha mshahara katika sekta binafsi kwa kushirikiana na wadau.

Sehemu ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani) wakati wa Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 63 wa mwaka wa Chama cha Waajiri uliofanyika Jijini Dodoma.

Prof. Ndalichako amesema katika Mwaka wa Fedha 2021/2022 Serikali ilipunguza mchango wa Waajiri katika Sekta Binafsi kwenye Mfuko wa Fidia ya Wafanyakazi kutoka asilimia 1 Hadi asilimia 0.6. Kuanzia Septemba 2021 Serikali ilipunguza adhabu ya kuchelewesha michango kwa mfuko wa fidia kwa Wafanyakazi kutoka asilimia 10 iliyokuwa ikitozwa kwa kila mwezi na kuwa asilimia 2.0 kwa mwezi.

Amefafanua kuwa, Waajiri wote waliokuwa wamechelewa kulipa michango yao kwa kipindi cha kuanzia tarehe 01 Oktoba, 2017 hadi tarehe 31 Agosti 2021 walisamehewa riba baada ya kulipa michango yao.

“Katika Bajeti Kuu ya Serikali kwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ambayo inaendelea kujadiliwa Bungeni Serikali, imependekeza kufuta tozo mbili za (OSHA) ambazo ni Tozo ya Sh 10,000 ya kipimo cha mzio, na Tozo ya Sh 25,000 ya kipimo cha kilele cha Upumuaji zilizokuwa zinatozwa kwa kichwa”.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Suzanne Ndomba – Doran, amebainisha kuwa chama hicho kitaendelea kushirikiana na serikali katika kudumisha ushirikiano wenye tija katika kuimarisha utatu wenye kujenga uchumi kwa Sekta za uzalishaji nchini.

Mkutano huo, ulihudhuriwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Patrobas Katambi, Mwenyekiti wa Bodi (ATE), Jayne Nyimbo Taylor, Rais wa (TUCTA), Tumaini Nyamhokhia, Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Colnel Magembe, Mwakilishi wa Mkurugenzi Ofisi ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) nchini Tanzania, Kenya, Rwanda na Uganda, Jealous Chirove, Kamishina wa Kazi, Bi.Suzan Mkangwa, Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi, Pendo Berege pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi – Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).

Dhima ya Mkutano huo ni: ‘Kuboresha Sera za Fedha na za Kodi ili kuongeza tija na kuchochea ukuaji wa Sekta za Kiuchumi.’

The post Waziri Ndalichako: Serikali inatambua mchango wa sekta binafasi katika kukuza uchumi appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/27562/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT