Skip to main content

Sudan: Maelfu ya kondoo wafariki baada ya meli iliyokuwa inawasafirisha Saudia kuzama

Meli hiyo ya mifugo ilikuwa inasafirisha wanyama hao kutoka Sudan kuelekea Saudi Arabia wakati ilipozama baada ya maelfu kadhaa ya wanyama zaidi kupakiwa ndani ya meli hiyo kuliko kiwango ilichotakiwa kubeba.

“Meli hiyo, Badr 1, ilizama mapema Jumapili asubuhi, afisa wa juu kwenye bandari amesema, akizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina.

“Ilikuwa imebeba kondoo 15,800, ambayo ni zaidi ya uwezo wake wa kupakia mizigo.”

Afisa huyo amesema meli hiyo ilikuwa inatakiwa kubeba kondoo 9,000 pekee.

Afisa mwingine, ambaye alisema wafanyakazi wote waliokolewa, ameelezea wasiwasi juu ya athari za kiuchumi na kimazingira za ajali hiyo.

“Meli hiyo iliyozama itaathiri shuguli za bandari,” amesema.

Ameongeza kuwa “huwenda ikasababisha pia athari za kimazingira kutokana na idadi kubwa ya wanyama waliokufa ambao walikuwa wamebebwa na meli hiyo.”

Omar al-Khalifa, mkuu wa chama cha kitaifa cha wanaosafirisha bidhaa nje, alisema meli hiyo ilifanya saa kadhaa kabla ya kuzama, ikimaanisha kuwa ingeweza kuokolewa.

Thamani ya jumla ya mifugo iliyoteketea ni takriban riyal za Saudia milioni 14, sawa na dola za Marekani milioni 4 , amesema Saleh Selim, mkuu wa kitengo cha mifugo kwenye chama hicho, akithibitisha pia kwamba kondoo hao walipakiwa kwenye meli hiyo katika bandari ya Suakin.

Amesema wenye mifugo walipata kondoo 700 pekee, lakini walikutwa wameumia sana na hawatarajii kwamba wataishi muda mrefu.

Selim ameomba uchunguzi ufanyike juu ya tukio hilo.

The post Sudan: Maelfu ya kondoo wafariki baada ya meli iliyokuwa inawasafirisha Saudia kuzama appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/23775/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT