Skip to main content

RC Mwanza aipongeza Ilemela kwa kupunguza hoja za CAG

Na Clara Matimo, Mwanza

Mkuu wa Mkoa  wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel, ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mkoani humo kwa kupunguza hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa asilimia 38 kwa mwaka wa fedha 2019/2020 hadi 2020/2021 pamoja na kupata hati safi kwa iaka sita mfululizo.

Mhandisi Gabriel ametoa pongezi hizo leo Jumatatu Juni 20, 2022 baada ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mhandisi Modest Apolinary, kusoma taarifa ya hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa nje (CAG) kwa mwaka wa fedha 2020/2021 pamoja na utekelezaji wake katika mkutano maalumu wa baraza la madiwani uliolenga kujadili hoja hizo.

Mhandisi Apolinary alisema katika kikao cha kupitia hoja za CAG  kwa mwaka wa fedha  2019/2020 halmashauri hiyo  ilikuwa na hoja 60  lakini katika kikao cha mwaka huu cha kupitia hoja za mwaka 2020/21 ina hoja 37  huku akifafanua kwamba zimepungua kwa asilimia 38 .

“Upungufu huo umetokana na usimamamizi mzuri wa kamati ya fedha, baraza la madiwani, ofisi ya mkuu wa wilaya na mkoa,  haya yote yameiwezesha halmashauri yetu ya manispaa ya Ilemela pia kupata hati safi kwa kipindi cha miaka sita mfululizo kuanzia mwaka wa fedha  2015/16 hadi 2020/2021.

“Sababu ya kupata hati hiyo ni ushirikiano baina ya wataalamu, madiwani, ofisi ya mkuu wa wilaya na mkoa katika kuhakikisha halmashauri inaendeshwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu, mwaka 2019/2020 hoja zilikuwa zimebaki 14, hoja sita zimefungwa, tatu ziko kwenye utekelezaji, tatu ni hoja za kujirudia  na mbili zimepitwa na wakati,” ameeleza Mhandisi Apolinary..

Aidha amefafanua kwamba zoezi la uhakiki kwa hoja tatu zilizo kwenye utekelezaji  kati ya 14 za miaka ya nyuma, 11 zimefungwa na  kwa mwaka wa fedha 2020/2021 hoja ni 23, kati ya hizo 13 zimefungwa, nane ziko kwenye utekelezaji, mbili ni za kujirudia.

“Hivyo, kati ya hoja 37 za miaka ya nyuma  na za mwaka 2020/2021,  26 zimefungwa  halmashauri imebaki na hoja 11 ambazo zote ziko kwenye hatua ya utekelezaji lengo letu ni kuhakikisha zote zinafungwa,”alisema.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masala, Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Kalli, alisema mwaka wa fedha 2022/2023 hawatakuwa na hoja hata moja ya kujibu kwani watakuwa makini zaidi kwa kufuata maelekezo na ushauri wa madiwani.

Baada ya maelezo hayo Mhandisi Gabriel aliwapongeza na kumuagiza mkurugenzi huyo kukaa na mkaguzi wa ndani  wajadiliane ili wafute hoja zote 11 zilizobaki  maana nyingi ni dhaifu huku akiwasisitiza kufuata ushauri watakaopewa na CAG.

The post RC Mwanza aipongeza Ilemela kwa kupunguza hoja za CAG appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/26165/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT