Skip to main content

RATIBA YA LIGI KUU BARA IPO HIVI


LEO Juni 25 Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea ambapo ratiba yake ni moto kwa timu zinazopambana kushuka daraja kwa kuwa hatma yao itaanza kufahamika leo.

Ni Yanga ambao ni mabingwa wa ligi wao hawana presha zaidi ya kuendelea kusaka rekodi za kutofungwa kwa msimu wa 2021/22 ndani ya ligi

Muziki kamili leo utakuwa namna hii:-Coastal Union v Kagera Sugar ngoma inapigwa saa 8:00 mchana.

Polisi Tanzania v Geita Gold hapa itapigwa saa 8:00 mchana.

Mbeya City v Yanga itapigwa saa 9:30 alasiri.

Biashara United v KMC ngoma itakuwa ni saa 10:00 jioni.

Mbeya Kwanza v Ruvu Shooting hizi zote zipo kwenye hatari ya kushuka daraja kwa kuwa Mbeya Kwanza ipo nafasi ya 16 na pointi 24 huku Ruvu Shooting ikiwa nafasi ya 13 na pointi 26 ngoma itapigwa saa 10:00 jioni.

Dodoma Jiji v Azam FC itapigwa saa 1:00 usiku.

Baada ya mechi za leo timu nyingi zitakuwa zimebakisha mchezo mmoja kukamilisha mzunguko wa pili msimu wa 2021/22.

The post RATIBA YA LIGI KUU BARA IPO HIVI appeared first on Saleh Jembe.

The post RATIBA YA LIGI KUU BARA IPO HIVI appeared first on soka letu.

Via soka letu https://ift.tt/z2IZnL9

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT